RAIS WA KENYA William Ruto Sasa Anadai Kuwa Hana Damu Mikononi Mwake Kufuatia Mauaji
Ya Watu Yaliyoshuhudiwa Wakati Wa Maandamano Ya Hivi Majuzi.
Kulingana
Na Ruto Ambaye Alikuwa Akizungumza Wakati Wa Kikao Na Wanahabari Katika Ikulu
Jumapili, Juni 30, Maafisa Wa Polisi Walitekeleza Majukumu Yao Kwa Njia Huru
Wakati Wa Maandamano Hayo.
Tume
Ya Haki Za Kibinadamu Ya Kenya (KHRC) Katika Rekodi, Imesema Watu 23 Walifariki
Kwa Kupigwa Risasi Na Polisi Kote Nchini. Zaidi Ya Hayo, Kulikuwa Na Zaidi Ya
Watu 50 Waliokamatwa, 22 Kutekwa Nyara, Na Zaidi Ya 300 Kujeruhiwa.Rais Ruto Hata
Hivyo Alishikilia Kuwa Ni Watu 19 Ndio Waliofariki.
Kuhusu
Hashtag Inayovuma Ya 'Ruto Lazima Aende', Rais Alisema Kila Mtu Ana Haki Ya
Kutoa Maoni Yake.
Rais
William Ruto Ameeleza Nia Yake Ya Kujihusisha Na Vijana Kwenye X Space.
Hii
Inafuatia Wito Wa Wakenya, Hasa Gen Z, Kwenye Mitandao Mbalimbali Ya Kijamii,
Ambao Wamesema Kwamba Ikiwa Mazungumzo Yoyote Yatafanyika Na Serikali, Yafanywe
Kwenye X Space.
Katika
Mahojiano Na Wanahabari Jumapili, Rais Alisema Yuko Tayari Kujadili Masuala
Yoyote Ambayo Wanaweza Kuwa Nayo.
“Nasikia
Vijana Wanasema Hatutaki Jukwaa La Sektambalimbali Labda Tufanye Mazungumzo Na Rais
Kwenye X. Mimi Niko Tayari Kufanya Mazungumzo Na Vijana Kwenye Jukwaa Hilo. Wakitaka
Nishirikiane Nao Kwenye X, Nitakuwepo," Alisema.
"Nataka
Tujadili Kuhusu Kodi, Nataka Tujadili Ukosefu Wa Ajira, Rushwa Na Masuala
Yote."
Vijana
Wamekuwa Wakiandaa Maandamano Nchini Kote Kwa Wiki Mbili Kuhusu Mswada Wa Fedha
Wa 2024, Ambao Ruto Alioundoa Kujibu Shinikizo Zinazoongezeka.
JISAJIRI
SASA NA PLAY MASTER BET - BETI KIRAHISI
BONYEZA
HAPA KUJISAJIRI