TANZANIA KUIUZIA ZAMBIA MAHINDI YA DOLA MILIONI 250

 


TANZANIA Itaiuzia Zambia Tani 650,000 Za Mahindi Katika Mpango Unaonuiwa Kusaidia Taifa Hilo La Kusini Mwa Afrika Kupunguza Uhaba Wa Chakula Unaosababishwa Na Ukame Wa Muda Mrefu.

Kupitia Mtandao Wa Kijamii Wa X, Waziri Wa Kilimo Hussein Bashe Amesema Nchi Hizo Mbili Zimetia Saini Makubaliano Ya Kusambaza Nafaka Hiyo, Inayotarajiwa Kulisha Takriban Watu Milioni 7.

 

Bashe Ameongeza Kuwa Makubaliano Hayo Na Zambia, Yatatekelezwa Ndani Ya Kipindi Cha Miezi Minane Huku Tanzania Ikipata Dola Milioni 250 Katika Biashara Hiyo.

 

Mkataba Huo Ulisainiwa Na Andrew Komba, Mkurugenzi Mkuu Wa Hifadhi Ya Chakula Ya Tanzania Inayomilikiwa Na Serikali (NFRA), Na Mratibu Wa Maafa Wa Zambia, Gabriel Poleni.

 

Zambia Inakabiliwa Na Ukame Ambao Umepunguza Uzalishaji Wa Umeme Na Chakula, Na Hivyo Kupelekea Serikali Kuagiza Chakula Kutoka Nchi Jirani.

JISAJIRI SASA NA PLAY MASTER BET - BETI KIRAHISI

BONYEZA HAPA KUJISAJIRI



Previous Post Next Post

ADVERT

ADVERT