MELI YA MV. CLARIAS Iliyokuwa
Kwenye Maegesho Ya Bandari Ya Mwanza Kaskazini Imekutwa Imepinduka Na Kuzama
Majini Katika Ziwa Victoria Asubuhi Ya Leo Mei 19, 2024, Huku Chanzo Cha Kuzama
Kwa Meli Hiyo Kikiwa Bado Hakijafahamika.
Meli Hiyo Ambayo Hivi
Karibu Ilikuwa Kwenye Matengenezo Bandari Ya Mwanza Kusini, Ilihamishiwa
Bandarini Hapo Tayari Kwa Kuanza Kutoa Huduma Za Usafiri Kwa Abiria Kati Ya Mwanza
Na Kisiwa Cha Ukerewe.
Hata Hivyo Inaelezwa Kuwa
Meli Hiyo Inaelezwa Haikua Na Abiria Yeyote Ndani.
Taarifa Zaidi Za Kuzama
Kwa Meli Hiyo Zitakujia Kadri Zitakavyopatikana.
Tags
LOCAL