WATU 11 Wamefariki Dunia
Na Wengine Wawili Kujeruhiwa Baada Ya Mfumo Wa Joto Wa Kiwanda Cha Kuzalisha
Sukari Cha Mtibwa Sugar Kulipuka Wakati Wakijiandaa Kuanza Uzalishaji Wa Sukari
Kwenye Kiwanda Hicho Kilichopo Turiani Mkoani Morogoro.
Akizungumza Na Mwananchi Digital
Leo Alhamisi Mei 23, 2024 Kamanda Wa Zimamoto Na Uokoaji Mkoa Wa Morogoro, Shaban
Marugujo Amesema Mlipuko Huo Ulitokea Saa 7 Usiku Na Umeua 11 Na Wengine Wawili
Kujeruhiwa.
"Ni Kweli Watu 11
Wamefariki Dunia Na Wengine Wawili Kujeruhiwa Baada Ya Mlipuko Wa Mpira
Wa Joto Wakati Wanajiandaa Na Uzalishaji Wa Sukari Pale Kiwandani,
Ifahamike Kwamba Ili Sukari Ichakatwe Kuna Kiwango Cha Joto Ambacho Kinatakiwa
Kifikie Sasa Wakati Maandalizi Ya Uzalishaji Yakifanyika Na Kile Kiwango Cha
Joto Kikingojewa Ndipo Ukatokea Mlipuko Huo Na Kuwakuta Watu Hao 11 Ambao Kwa
Kiwango Kile Cha Joto Wakafariki Papo Hapo,"
"Chanzo Halisi Cha
Mlipuko Huo Bado Hatujakipata Ila Bado Tunaendelea Na Uchunguzi, Timu Nzima Iko
Hapa Kiwandani Tangu Usiku Huo Na Mpaka Sasa Tunaendelea Na Tukikamilisha
Tutatoa Taarifa Rasmi" Amesema Marugujo.