TETESI ZA SOKA ULAYA JUMANNE MEI 22 2024

MANCHESTER CITY Wako Tayari Kutoa Ofa Kwa Mlinda Lango Wa Brazil Ederson, 30, Ambaye Anavutiwa Na Saudi Arabia. (Fabrizio Romano)

Manchester United Inachunguza Uwezekano Wa Kumsajili Mlinzi Wa Crystal Palace Na England Marc Guehi, 23, Ikiwa Watashindwa Kufikia Makubaliano Na Everton Kumnunua Beki Wa Kati Wa England Jarrad Branthwaite, 21(Mail)

Manchester United Wako Katika Nafasi Ya Kutumia Fedha Nyingi Katika Dirisha La Usajili La Majira Ya Joto Huku Hasara Kubwa Katika Miaka Ya Hivi Karibuni Sasa Ikiwaacha Nje Ya Kanuni Za Faida Na Uendelevu (PSR). (Football Insider)

Arsenal, Manchester United Na Liverpool Wamefanya Mawasiliano Na Benfica Kuhusu Uwezekano Wa Kumnunua Beki Wa Kati Wa Ureno Antonio Silva, 20. (Caught Offside)

Meneja Mpya Wa Liverpool Arne Slot Amemweka Kiungo Wa Kati Wa Benfica Na Uturuki Orkun Kokcu, 23, Juu Ya Orodha Yake Ya Wachezaji Anaotaka Kuwasajili (Givemesport)

Thomas Tuchel Amefanya Mazungumzo Na Chelsea Kuhusu Kurejea Katika Klabu Hiyo Kwa Kipindi Cha Pili. (Florian Plettenberg)

Manchester United Wanaweza Kubadilisha Meneja Wao, Wakati Manchester City Wanafikiria Kumruhusu Mchezaji Nyota Kuondoka ...

Mauricio Pochettino Yuko Kwenye Rada Ya Manchester United Na Bayern Munich Baada Ya Kuondoka Chelsea Kwa "Makubaliano Ya Pande Zote".(Standard),

Meneja Wa Stuttgart Sebastian Hoeness Na Kieran Mckenna Wa Ipswich Town Wametajwa Na Chelsea Kama Wanaoweza Kuchukua Nafasi Ya Pochettino(Teamtalk)

Mkufunzi Wa Girona Michel Na Enzo Maresca Wa Leicester City Pia Huenda Wakawa Miongoni Mwa Majina Yanayozingatiwa Na Chelsea .(Daily Telegraph )

Arsenal Wataanzisha Kipengele Cha Chaguo Lao La Kumnunua Mlinda Lango Wa Uhispania David Raya, 28, Na Kufanya Uhamisho Wake Wa Mkopo Kutoka Brentford Kuwa Wa Kudumu Msimu Huu Kwa Pauni Milioni 27. (Football Insider)

Tottenham Wameiuliza Chelsea Kuhusu Kupatikana Kwa Trevoh Chalobah, 24, Wakati Wakijiandaa Kuanzisha 'Uvamizi' Mara Dufu Kuipata Sahihi Ya Beki Wa Uingereza Conor Gallagher, 24. (HITC).

Manchester United Na Bayern Munich Zilituma Maskauti Kumtazama Kiungo Wa Mali Mwenye Umri Wa Miaka 18, Malick Junior Yalcouye Akiichezea IFK Gothenburg Katika Ushindi Wa 1-0 Dhidi Ya Mjallby Siku Ya Jumanne. (Expressen - Kwa Kiswidi)

Aston Villa Wamewasilisha Ombi La £12.8m Kwa Sevilla Kumnunua Beki Wa Argentina Marcos Acuna, 32. (Fichajes - Kwa Kihispania)

Villa Pia Wanavutiwa Na Mlinzi Wa Italia Raoul Bellanova, 24, Baada Ya Kuonyesha Kiwango Kizuri Msimu Wake Wa Kwanza Akiwa Na Torino , Lakini West Ham Na Manchester United Pia Wana Hamu Ya Kumnunua (Tuttosport - Kwa Kiitaliano)

West Ham Wanafikiria Kumnunua Serhou Guirassy, ​​28, Baada Ya Mshambuliaji Huyo Wa Guinea Kuifungia Stuttgart Mabao 28 Ya Bundesliga Msimu Huu. (Standard)

Tottenham Itapambana Na Aston Villa Kwa Ajili Ya Kumnunua Beki Wa Italia Andrea Cambiaso, 24, Ambaye Juventus Inasema Thamani Yake Ni Pauni Milioni 34 (Calciomercato - Kwa Kiitaliano)

Fulham Na West Ham Wamefanya Mazungumzo Na Corinthians Kuhusu Uwezekano Wa Kumsajili Mshambuliaji Wa Brazil Wesley Mwenye Umri Wa Miaka 19(Caught Offside)

Previous Post Next Post

ADVERT

ADVERT