CHADEMA WAVURUGANA NA KUHARIBU UCHAGUZI NJOMBE


UCHAGUZI Wa Kumpata Mwenyekiti Wa Mkoa Wa Njombe, Uliowakutanisha Rose Mayemba Na Ahadi Tweve Umevunjika Baada Ya Kutokea Ugomvi Baina Ya Pande Mbili Zinazowaunga Mkono Wagombea Hao.

Uchaguzi Huo Ulivunjika siku ya jana Ijumaa Mei 24,2024 Baada Ya Kutokea Sintofahamu Iliyosababishwa Na Wanachama Waliodai Kuwa Kuna Baadhi Ya Wajumbe Kutoka Wilayani Makete Hawakupaswa Kushiriki Mchakato Huo Kwa Kuwa Si Wajumbe Halali.

Mwenyekiti Wa Chadema Kanda Ya Nyasa, Mchungaji Peter Msigwa Amesema Kuwa  Uchaguzi Huo Umevurugika Baada Ya Baadhi Ya Wanachama Kuleta Vurugu.

"Ni Kweli Uchaguzi Umevurugika, Hawa Waliosababisha Ni Wale Miongoni Mwa Makundi Yaliyoshindwa Wakati Ule, Wamesababisha Vurugu Na Uchaguzi Umeahirishwa Hadi Hapo Utaratibu Utakapotangazwa Tena," Amesema Msigwa. 
Mmoja Wa Wanachama Wa Chama Hicho, Mkoa Wa Njombe, Jimy Sanga  Amedai Kuwa Vurugu Hizo Zilianza Baada Ya Wanachama Kudai  Kuwa Wajumbe Kutoka Jimbo La Makete Si Halali.

"Uchaguzi Ukasitishwa Ghafla Wengine Walikuwa Wanasema  Umeshindwa Kufanyika Kutokana  Na Mkanganyiko Wa Katiba. Sasa Mambo Mengi Yamejitokeza Tunasubiri Utaratibu Wa Chama Kitakuja Na Muongozo Gani," Amesema.

Kada Mwingine Ambaye Hakutaka Jina Lake Litajwe, Amedai Mchakato Huo Umeahirishwa Kwa Sababu Ya Vurugu Zilizotokana Na Wajumbe Wa Upande Mmoja Kupinga Viongozi Wa Jimbo La Makete Kushiriki Uchaguzi Huo Mkoa.

"Rufaa Ya Kupinga Uchaguzi Wa Jimbo La Makete Iliamuliwa Na Kamati Kuu Ambayo Imesema Wajumbe Hao Hawana Uhalali Hivyo Uchaguzi Wa Makete Haukuwa Halali," Amesema Kada Huyo.

Mei 17, Mwaka Huu Mkurugenzi Wa Itifaki, Mawasiliano Na Mambo Ya Nje Wa Chadema, Alisema Kikao Cha Kamati Kuu Kilichoketi Mei 11 Hadi 14 Kilijadili Taarifa Za Rufaa Mbalimbali Ikiwemo Rufaa Za Uchaguzi Wa Mkoa Wa Njombe Uliofutwa Na  Kamati Maalumu .

Mrema Amesema Kamati Kuu Iliufuta Uchaguzi Huo Kutokana Na Uchaguzi Huo Kuendeshwa Bila Kufuata Katiba Na Kanuni Za Kusimamia Chaguzi Ndani Ya Chama Hicho Kikuu Cha Upinzani.

"Kamati Kuu Ilikubaliana Na Sababu Za Kufutwa Uchaguzi Huo Na Kuagiza Ufanyike Upya  Na  Hapatakuwa Na Uchukuaji Wa Fomu Upya Wala Usaili Bali Wagombea Walewale Walioshiriki Duru Ya Kwanza Ndio Watakaogombea," Amesema Mrema.

Hata Hivyo, Leo Mwananchi Imemtafuta  Mrema Ambaye Amesema Atafutwe Baada Ya Muda. 
Usiku Huu Ametafutwa Tena Amesema Atatoa Majibu Baadaye.

Previous Post Next Post

ADVERT

ADVERT