MVUA Kubwa Zilizonyesha
Nchini Kenya, Tanzania Na Mataifa
Jirani Zilisababisha Vifo Vya Zaidi Ya Watu 500, Na Kuwalaazimu
Mamia Ya Maelfu Kuyahama Makazi Yao Huku Mafuriko Yakisomba Nyumba Na Kuvunja
Barabara Wakati Wa Msimu Wa Masika Kuanzia Mwezi Machi Hadi Mei.
Kanda Hiyo Pia Ilikumbwa
Na Mafuriko Mwishoni Mwa Mwaka Jana, Huku Watafiti Wakisema Kuwa Dipole Ya Bahari
Ya Hindi (IOD), Ambayo Ni Mfumo Wa Hali Ya Hewa Unaofafanuliwa Na Tofauti
Ya Joto La Uso Wa Bahari Kati Ya Maeneo Ya Magharibi Na Mashariki Mwa Bahari --
Ilichangia Mvua Kubwa.
Mvua Za Mwaka Huu
Ziliaminika Kuwa Zilichochewa Zaidi Na El Nino -- Hali Ya Hewa Inayohusishwa Na
Ongezeko La Joto Ambalo Husababisha Ukame Katika Baadhi Ya Maeneo Ya Dunia Na
Mvua Kubwa Kwingineko.
Lakini Utafiti
Uliochapishwa Na Shirika La World Weather Attribution (WWA) Siku Ya Ijumaa Uligundua
Kuwa "Watafiti Hawakupata Ushahidi Wowote Kwamba El Nino Au Dipole Ya Bahari
Ya Hindi Vilikuwa Na Ushawishi Wowote" Juu Ya Mvua Kubwa Za Mwaka Huu.
Mtandao Huo Wa
Wanasayansi Umebuni Mbinu Zilizopitiwa Na Wataalamu Wenzao Kwa Ajili Ya
Kubainisha Kwa Haraka Jukumu Linalowezekana La Ongezeko La Joto Duniani Katika
Matukio Mahususi Ya Hali Ya Hewa Kali.
Wanasayansi Walichunguza
Data Za Hali Ya Hewa Na Mifano Ya Tabianchi Ili Kulinganisha Jinsi Mifumo Ya
Mvua Ilivyobadilika Kati Ya Sasa Na Enzi Ya Kabla Ya Viwanda, Wakitafuta Kupima
Athari Za Mabadiliko Ya Tabianchi Kwa Monsuni.
Sababu
Mchanganyiko
"Mvua Iliyokithiri
Iliyosababisha Mafuriko Makubwa Nchini Kenya, Tanzania Na Maeneo Mengine Ya Afrika Mashariki Inazidi Kuwa
Kubwa, Huku Mabadiliko Ya Tabianchi Yakiwa Moja Ya Vichochezi," Watafiti
Walisema.
"Makadirio Bora
Zaidi Ni Kwamba Mabadiliko Ya Htabianchi Yalifanya Tukio Hilo Kuwa Mara Mbili
Zaidi Na Asilimia Tano Kuwa Kali Zaidi," Walisema, Na Kuongeza Tahadhari
Kwamba Matokeo Hayo Pia Yalipaswa Kuzingatia "Mashaka Makubwa Ya
Kihesabu".
Utafiti Huo Ulihusu
"Kiwango Cha Juu Cha Mvua Kwa Siku 30" Katika Msimu Wa Masika Wa
Mwaka Huu, Huku Watafiti Wakieleza Kuwa "Mvua Kubwa Itaendelea Kuongezeka
Katika Eneo Hilo Kutokana Na Ongezeko La Joto."
Utafiti Huo Umezitaka
Serikali Katika Eneo Hilo Kuboresha Miundombinu Na Kulinda Mifumo Ya Ikolojia
Ili Kuokoa Maisha Na Kuwasaidia Wananchi Kukabiliana Na Hatari Kubwa Ya Majanga
Ya Hali Ya Hewa, Hasa Katika Maeneo Ya Mijini Yenye Watu Wengi.
Afrika Mashariki Na Pembe
Ya Afrika Ni Miongoni Mwa Maeneo Yaliyo Hatarini Zaidi Na Mabadiliko Ya
Tabianchi -- Ingawa Mchango Wa Bara La Afrika Katika Utoaji Wa Hewa Ukaa
Duniani Ni Sehemu Ndogo Tu Ya Utoaji Jumla Wa Gesi Hiyo Duniani.
Zaidi Ya Watu 300
Walikufa Kutokana Na Mvua Na Mafuriko Nchini Ethiopia, Kenya Na Somalia Mwishoni
Mwa Mwaka Jana, Wakati Eneo Hilo Lilipokuwa Likijaribu Kujikwamua Kutokana Na
Ukame Mbaya Zaidi Katika Miongo Minne Iliyoacha Mamilioni Ya Watu Wakikabiliwa
Na Njaa.
Utafiti Wa WWA Kuhusu
Mafuriko Ya Mwaka Jana Katika Kanda Ya Afrika Mashariki Ulitoa Wito Wa
Kukomeshwa Kwa Haraka Kwa Nishati Ya Mafuta Na Kupunguza Utoaji Wa Hewa Chafu
Duniani Kote.