RAIS WA IRAN Ebrahim
Raisi Pamoja Na Waziri Wa Mambo Ya Nje Wa Nchi Hiyo Hossein Amir-Abdollahian Na
Wengine Kadhaa Wamethibitishwa Kufariki Dunia Katika Ajali Ya Helikopta
Iliyotokea Jana Jumapili Kaskazini-Magharibi Mwa Iran Hii Ni Kwa Mujibu Wa
Runinga Ya Taifa Hilo.
Taarifa Za Awali
Zilieleza Kuwa Hali Mbaya Ya Hewa Ikiwemo Ukungu Katika Eneo Ilipotokea Ajali
Hiyo, Ulifanya Helikopta Hiyo Kushindwa Kutua Wakati Rais Huyo Na Ujumbe Wake
Wakielekea Mji Wa Tabriz Uliopo Kaskazini Magharibi Mwa Iran.
Shirika La Kimataifa La Msalaba
Mwekundu Mapema Leo Waokoaji Walilipata Eneo Ilipoanguka Helikopta Hiyo Na
Kuelezwa Kwamba Ulikuwa Imeteketea Kabisa.
Helikopta Hiyo Ni Miongoni
Mwa Helikopta Tatu Zilzokuwa Katika Msafara Huo, Ambapo Mbili Inaelezwa Zilitua
Salama.