KWA NINI VIKOSI VYA TANZANIA VIKO MSUMBIJI, DRC?

WAZIRI Wa Mambo Ya Nje Na Ushirikiano Wa Afrika Mashariki, January Makamba, Amesema Tanzania Haitachoka Kupeleka Askari Wake Kulinda Amani Katika Nchi Za Jumuiya Ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika (Sadc) Kwa Sababu Inaamini Katika Uhusiano Wa Kindugu, Uliowekwa Na Waasisi Wa Taasisi Hiyo.

Akizungumza Na Mabalozi Wa Nchi Za Sadc Wanaowakilisha Nchi Zao Jijini Beijing, China Jana, Makamba Alisema Msingi Huo Wa Kifalsafa Ndiyo Uliofanya Tanzania Sasa Iwe Na Askari Katika Nchi Za Jamhuri Ya Kidemokrasia Ya Congo (DRC) Na Msumbiji Baada Ya Kuombwa Kufanya Hivyo Na Nchi Wenyeji.

“Nimekuja Hapa Kuzungumza Nanyi Na Kuwahakikishia Kwamba Msimamo Wa Tanzania Kuhusu Sadc Haujawahi Kuyumba Na Hautabadilika. Tatizo Lolote Litakaloikumba Nchi Ya Sadc Litachukuliwa Kuwa Pia Ni Tatizo La Tanzania Wakati Wote,” Alisema.

Makamba Ambaye Yuko Katika Ziara Ya Kikazi Nchini China Kufuatia Mwaliko Aliopewa Na Mwenyeji Wake Ambaye Ni Waziri Wa Mambo Ya Nje Wa China, Wang Yi, Alisema Sadc Ni Jumuiya Imara Kulinganisha Na Nyingine Kwa Sababu Msingi Wake Ulijengwa Katika Falsafa Na Misingi Imara.

Akizungumza Kwa Niaba Ya Mabalozi Wa Nchi 14 Za Sadc Waliohudhuria Mkutano Huo, Balozi Wa Namibia Nchini China, Elia Kaiyamo, Alisema Wamefurahi Kusikia Maneno Ya Makamba Kwa Vile Yameakisi Maneno Yaliyowahi Kutamkwa Zamani Na Baba Wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere Kuhusu Umuhimu Wa Nchi Za Sadc Kuwa Pamoja.

Baadhi Ya Nchi Za Sadc Ambazo Vikosi Vya Tanzania Vimekwenda Kuimarisha Ulinzi Ni Pamoja Na Msumbiji Na DRC Ambako Hadi Sasa Kuna Vikosi Vya Askari Wa Tanzania Wanaoimarisha Ulinzi Na Usalama.

Previous Post Next Post

ADVERT

ADVERT