TAIWAN imemwapisha Lai
Ching-te kuwa rais mpya wa kisiwa hicho katika hafla iliyohudhuriwa na
viongozi kadhaa wa kimataifa. Lai, ambaye amewahi kushikilia nafasi ya makamu
wa rais chini ya rais anayeondoka Tsai Ing-wen, amekula kiapo leo katika ofisi
ya rais na kisha kufuatiwa na uapisho wa naibu wake Hsiao Bi-khim.
Lai, anaingia madarakani,
mnamo wakati China ikizidisha shinikizo la kijeshi na kisiasa dhidi ya kisiwa
hicho kinachojitawala. China inadai kwamba Taiwan ni sehemu ya himaya yake na
imemtaja Lai kuwa "mtu hatari anayetaka kujitenga" na ambaye
atasababisha mvurugano dhidi ya kisiwa hicho.
Kama ilivyokuwa kwa
mtangulizi wake Ing-wen, Lai ni mtu anayepigia upatu demokrasia ya kisiwa hicho
na katika kipindi cha nyuma amewahi kujinasibu kama mtu wa vitendo katika uhuru
wa Taiwan.