MAFURIKO MAPYA YASABABISHA VIFO VYA WATU 66 AFGHANISTAN

 


MAFURIKO Mengine Mapya Yamewaua Watu 66 Katika Mkoa Wa Faryab Kaskazini Mwa Afghanistan. Mamia Ya Watu Wamekufa Katika Mafuriko Tofauti Mwezi Huu Ambayo Pia Yamesomba Mashamba Katika Nchi Hiyo Ambayo Asilimia 80 Ya Wakazi Wanategemea Kilimo.

Zaidi Ya Nyumba 1,500, Na Ekari Zaidi Ya 1,000 Vimeharibiwa. Mafuriko Hayo Yametokea Siku Moja Baada Ya Zaidi Ya Watu 50 Kufariki Katika Mafuriko Mengine Kwenye Mkoa Wa Magharibi Wa Ghor.

Zaidi Ya Wiki Moja Iliyopita, Watu Wengine Zaidi Ya 300 Walikufa Kwenye Mafuriko Yaliyolikumba Jimbo La Kaskazini La Baghlan, Kulingana Na Shirika La Mpango Wa Chakula La Umoja Wa Mataifa WFP Na Maafisa Wa Taliban.

Maafisa Wa Taliban Wameonya Kwamba Idadi Ya Vifo Huenda Ikaongezeka Katika Mikoa Iliyoathiriwa Na Mafuriko, Kwani Miundombinu Iliyoharibiwa Inatatiza Utoaji Wa Misaada Na Juhudi Za Uokoaji.

Previous Post Next Post

ADVERT

ADVERT