RAIS
Wa Kenya William Ruto Alikuwa Washington Kwa Ziara Ya Kiserikali
Wakati Ikulu Ya Marekani Ilipoahidi Ushirikiano Mpya Kuhusu Teknolojia, Usalama
Na Msamaha Wa Madeni Kwa Demokrasia Hiyo Ya Afrika Mashariki.
"Wawekezaji Wanapenda
Kile Wanachokiona Nchini Kenya," Ruto Alisema, Akiwavutia Viongozi Wa
Biashara Kwenye Hafla, Na Kuahidi Kurahisisha Ufanyaji Biashara.
Waziri Wa Biashara Wa Marekani
Gina Raimondo Aliwataka Viongozi Wa Biashara Kudumisha Kasi Baada Ya Matukio Ya
Wiki. "Hatuwezi Kwenda Nyumbani, Kufurahishwa Na Wikendi Na
Kuendelea," Raimondo Alisema. "Sote Tuko Afrika, Sote Nchini Kenya. Twende
Kufanya Mikataba Zaidi Pamoja."
Ofisi Ya Mwakilishi Wa Biashara Wa Marekani Ilisema
Kuwa Nchi Hizo Zitafanya Duru Ya Sita Ya Mazungumzo Ya Ana Kwa Ana Chini Ya Ubia
Wa Kimkakati Wa Biashara Na Uwekezaji (STIP) Mjini Mombasa Kuanzia Juni 3 Hadi
7 Baada Ya Duru Ya Mjini Washington Mwezi Huu.
Soma Pia: Biden, Ruto Waahidi Kulinda Demokrasia Afrika
Na Kwingineko
Ruto Alisema Ameshughulikia
Wasiwasi Ulioibuliwa Na Kampuni Ya Google Ya Alphabet Ili Kurahisisha
Operesheni Zake, Na Kuorodhesha Sera Kadhaa Za Ushuru Na Nyingine Ili
Kuhimiza Uwekezaji Wa Moja Kwa Moja Wa Kigeni.
Google,
Miscrosoft Zaongoza Uwekezaji
Rais Wa Alphabet Na Afisa
Mkuu Wa Uwekezaji Ruth Porat Alisema Ijumaa Kwamba Google Inakuza Uwekezaji
Nchini Kenya, Ikiwa Ni Pamoja Na Katika Ushirikiano Wa Kujenga Njia Ya Kwanza
Kabisa Ya Fiber Optic Kuiunganisha Afrika Moja Kwa Moja Na Australia, Ambayo
Inapitia Barani Humo Hadi Afrika Kusini Kabla Ya Kuvuka Bahari Ya Hindi Hadi Australia.
Ruto Aliongeza Kuwa Kenya
Imekuwa Ikifanya Kazi Kuvutia Makampuni Makubwa Ya Teknolojia Na Kampuni Changa
Kupitia "Silicon Savannah" Yake Na Kuongeza Kwamba Kenya Inalenga
Katika Utengenezaji Wa Magari Ya Kielektroniki.
"Serikali Ya Kenya Katika
Mfumo Ujao Wa Sera Tutakuwa Tukiondoa Ushuru Wote Kwa Kampuni Ambazo
Zitatengeneza Vyombo 100,000 Vya Kwanza Vya Magurudumu Mawili Na Magurudumu
Manne Nchini Kenya," Ruto Alisema.
Shirika La Ufadhili Wa Maendeleo
Ya Kimataifa La Marekani Wiki
Hii Lilitangaza Mkopo Wa Moja Kwa Moja Wa Dola Milioni 10 Kwa Basigo, Kampuni
Ya Magari Ya Umeme Inayokodisha Na Kuuza Mabasi Ya Umeme Kwa Waendeshaji Wa
Mabasi Ya Usafiri Wa Umma Nchini Kenya Na Mkopo Wa Dola Milioni 10 Kwa Kampuni
Ya Kenya Ya Roam Electric Kusaidia Utengenezaji Wa Pikipiki Za Umeme Jijini Nairobi.
Soma Pia: Biden, Ruto Kujadili Msamaha Wa Deni Kwa Kenya
Wiki Hii
Miongoni Mwa Mikataba
Iliyotiwa Saini Siku Ya Ijumaa Ni Pamoja Na Ushirikiano Wa Kenya Na Microsoft Wa
Kujenga Kituo Cha Kuhifadhi Data Cha Gigawati 1 Chenye Thamani Ya Dola Bilioni
1 Mjini Naivasha, Kenya Ambacho Kitatumia Huduma Za Azure Cloud Za Kampuni Ya Microsoft
Kwa Ajili Ya Programu Zinazotegemea Teknolojia Ya Cloud.
Hatua Hiyo Itaruhusu
Serikali Ya Kenya Kuhamisha Data Na Huduma Zake Kwa Wachuuzi Wanaoaminika,
Ilisema Ikulu.
Rais Wa Microsoft Brad
Smith Alisema Chini Ya Ushirikiano Kampuni Hiyo Itasaidia Kuleta Huduma Za
Mtandao Kwa Watu Milioni 20 Mwaka Ujao Nchini Kenya.