ALIYEKUWA Mbunge Wa Mbeya
Mjini, Joseph Mbilinyi, Maarufu Sugu Ameibuka Mshindi Wa Nafasi Ya Mwenyekiti Wa
Chama Cha Demokrasia Na Maendeleo (Chadema), Kanda Ya Nyasa Akimbwaga Mpinzani
Wake Mchungaji Peter Msigwa.
Sugu Amemshinda Msigwa Ambaye
Alikuwa Anatetea Nafasi Yake Kwa Kura 54 Kwa 52 Na Sasa Kada Huyo Ataiongoza
Kanda Hiyo Kwa Miaka Mitano Hadi 2029.
Akitangaza Matokeo Hayo
Jana Mei 29, 2024 Msimamizi Wa Uchaguzi Huo,
Kaimu Katibu Mkuu Wa Chama Hicho Bara, Benson Kigaila Amesema Jumla Ya
Wapiga Kura Walikuwa 106 Na Hakuna Kura Zilizoharibika.
Akizungumza Baada Ya
Matokeo Hayo, Msigwa Amewashukuru Wapiga Kura Kwa Maamuzi Yao Akieleza Kuwa
Thamani Yake Itabaki Vilevile Bila Kuwa Kiongozi.
Amesema Ataendelea
Kukitumikia Chama Kwani Hakuingia Chadema Kwa Ajili Ya Uongozi Na Kumpongeza Sugu
Kwa Kushinda Na Kumuahidi Ushirikiano Pale Atakapohitaji Msaada Wake.
"Niwashukuru Sana Wajumbe
Kwa Uamuzi Wenu Mmetaka Mabadiliko Na Ninapokea Vyema Matokeo, Naamini Thamani
Yangu Kichama Itabaki Hivyo Nimpongeze Sugu Na Niko Tayari Kwa Ushirikiano
Popote Nitakapohitajika" Amesema Msigwa.
Naye Sugu Mbali Na
Kutanguliza Shukurani Amesema Wapiga Kura Kuridhia Na Kumpa Kura Za Kutosha Inaakisi Wajumbe Kukubaliana
Na Ajenda Zake 10, Hivyo Kwa Peke Yake Hatoweza Akiomba Ushirikiano.
Amesema Kwa Sasa Suala Ni
Moja Kuwaunganisha Wanachama Haswa Kwa Kipindi Hiki Wakielekea Uchaguzi Wa Serikali
Za Mitaa Na Uchaguzi Mkuu Na Kwamba Ili Awe Bora Anahitaji Viongozi Bora
Kuanzia Mkoa, Wilaya Na Majimbo.
"Yale Mazuri
Uliyofanya Msigwa Nitayachukua, Lengo
Letu Ni Kukipa Thamani Chama Na Kuwaunganisha Wote, Kuanzia Kesho Mei 30,2024 Tunaanza Upya Kwani Sijashinda Mimi Bali
Chama Ndicho Kimeshinda" Amesema Sugu.
Katika Nafasi Ya Makamu Mwenyekiti Kanda Ya Nyasa, Amepita Frank Mwakajoka,
Huku Nafasi Ya Mweka Hazina Akishinda Grace Shio.