OPERESHENI YA ISRAEL MJINI RAFAH HAIJAVUKA MSTARI MWEKUNDU WA MAREKANI- WHITE HOUSE

MAREKANI Haiamini Kuwa Israel Imeanzisha Uvamizi Kamili Wa Rafah Kusini Mwa Gaza, Msemaji Wa Ikulu Ya Marekani John Kirby Amesema.

Alizungumza Saa Chache Baada Ya Vikosi Vya Israel Kufika Katikati Mwa Mji Huo Na Kuripotiwa Kukamata Kilima Muhimu Kimkakati Kinachotazamana Na Mpaka Wa Karibu Na Misri.

Rais Wa Marekani Joe Biden Alisema Hapo Awali Uvamizi Katika Mji Wa Rafah, Ambapo Mamia Ya Maelfu Ya Raia Bado Wanafikiriwa Kuwa Wamejikinga, Utavuka Mstari Mwekundu.

Bw. Kirby Pia Alihojiwa Kuhusu Shambulizi La Anga La Israel Na Kusababisha Moto Uliosababisha Vifo Vya Wapalestina 45 Katika Kambi Moja Ya Watu Waliokimbia Makazi Yao Siku Ya Jumapili.

Israel Imesema Inaamini Kuwa Moto Huo Unaweza Kusababishwa Na Silaha Zilizohifadhiwa Katika Maeneo Ya Jirani Na Hamas Kulipuka.

Bw. Kirby Aliwaambia Waandishi Wa Habari Kwamba Picha Za Shambulio La Jumapili, Ambalo Liliua Wanawake Wengi, Watoto Na Wazee, "Zinavunja Moyo" Na "Za Kutisha".

"Hapapaswi Kuwa Na Maisha Yasiyo Na Hatia Yanayopotea Hapa Kutokana Na Mzozo Huu," Aliongeza.

Lakini Alikiri Kuwa Israel Inachunguza Tukio Hilo Na Kusema "Hana Mabadiliko Ya Kisera Ya Kuzungumza Nayo" Kufuatia Matukio Ya Hivi Karibuni Huko Rafah.

"Bado Hatuamini Operesheni Kubwa Ya Ardhini Inafaa ... Na Hatujaona Hilo Kwa Wakati Huu," Alisema.

Rais Biden Alisema Mapema Mwezi Huu Kwamba Baadhi Ya Usambazaji Wa Silaha Kwa Israel Utasitishwa Iwapo Kutakuwa Na Operesheni Kubwa Ya Ardhini Huko Rafah.

Waziri Mkuu Wa Israel Benjamin Netanyahu Ameelezea Shambulio La Jumapili Kama "Bahati Mbaya", Huku Akiapa Kuendeleza Operesheni Ya Rafah.

Jeshi La Israel Limesema Shambulio Hilo Lililenga Na Kuwaua Maafisa Wawili Wakuu Wa Hamas.

Siku Ya Jumanne, Ilisema Wanajeshi Wake Walikuwa Wakiendelea Na Shughuli Dhidi Ya "Maeneo Ya Magaidi" Huko Rafah, Wiki Tatu Baada Ya Kuanzisha Operesheni Ya Ardhini Huko.

Walioshuhudia Walisema Vifaru Vya Israel Vilikuwa Vinazunguka Al-Awda,

Maeneo Ya Magharibi Ya Jiji Yalikumbwa Na Mashambulizi Makali Ya Mabomu Usiku Wa Kuamkia Jumatatu Hadi Jumanne, Wakaazi Walisema.

Jeshi La Israel Limekanusha Ripoti Siku Ya Jumanne Kwamba Mizinga Ya Vifaru Vyake Vilipiga Kambi Nyingine Ya Hema Huko Al-Mawasi, Pwani Ya Magharibi Ya Rafah, Ambayo Maafisa Wa Eneo Hilo Walisema Kuwa Imewauwa Takribani Watu 21.

Video Za Tukio Hilo Zilizochapishwa Kwenye Mitandao Ya Kijamii Na Kuchambuliwa Na BBC Verify Zilionesha Watu Wengi Wakiwa Na Majeraha Mabaya.

Hakukuwa Na Dalili Za Wazi Ya Eneo La Mlipuko, Na Hivyo Kufanya Kutowezekana Kufahamika Sababu Ya Tukio Hilo.

Previous Post Next Post

ADVERT

ADVERT