RIPOTI MPYA Inasema Kuwa
Dhahabu Ya Thamani Ya Mabilioni Ya Dola Inasafirishwa Kimagendo Kutoka Afrika Kila
Mwaka.
Uchunguzi Wa Shirika La Swissaid
Umegundua Kuwa Nyingi Ya Dhahabu Hiyo Huishia Kati Umoja Wa Falme Za Kiarabu.
Swissaid Imesema Umoja Huo
Wa Falme Za Kiarabu Ndio Kituo Kikuu Cha Dhahabu Hiyo Kutoka Afrika Ambako Mji
Wa Dubai Unatambulika Kwa Kuwa Na Soko Kubwa La Dhahabu,Kisha Badaye
Husafirishwa Hadi Nchi Za Ulaya Kama Uswisi,India Na Nyingine Huishia Marekani.
Ripoti Hiyo Inasema Mali,
Zimbabwe Na Ivory Coast Zinazalisha Kiasi Kikubwa Zaidi Cha Dhahabu Ambayo
Haisajiliwi Rasmi.
Inakadiriwa Kuwa Karibu
Asilimia Arobaini Ya Dhahabu Ya Afrika Husafirishwa Nje Ya Bara Hilo Kimagendo
Na Kiwango Kimeongezeka Mara Mbili Katika Kipindi Cha Muongo Mmoja Uliopita.
Tani Kati Ya Mia Tatu Na
Mia Nne Za Dhahabu Za Thamani Ya Hadi Dola Bilioni Thelathini Na Tano
Zinazozalishwa Katika Migodi Midogo Hazijulikani Zinakoishia Kila Mwaka.
Shirika Hilo La Swissaid Linasema
Madini Hayo Yenye Thamani Kubwa Ni Chanzo Cha Vipato Kwa Wachimba
Madini,Upatikanaji Wa Kodi Kwa Serikali Nyingi Za Afrika,Lakini Pia Huchangia
Katika Kufadhili Makundi Ya Waasi Na Kuchangia Katika Vitendo Vya Uvunjifu Wa
Haki Za Binadamu Na Uchafuzi Wa Mazingira.
Ripoti Hiyo Inaangazia Kipindi Cha Kati Ya Mwaka 2012 Na 2022 Na Inajikita Katika Data Zilizokusanywa Kutoka Nchi 54.