VINCENT KOMPANY Amechaguliwa
Kuwa Kocha Ajaye Wa Bayern Munich Lakini Maelezo Kuhusu Mkataba Wake Bado
Yanapaswa Kukamilishwa.
Mwanachama Wa Bodi Ya
Klabu Hiyo Karl-Heinz Rummenige Amesema Mkurugenzi Wa Spoti Wa Klabu Ya Bayern
Munich Max Erbel Amemchagua Kompany Kuwa Kocha Mpya.
Rummenige, Ambaye Ni
Mshambuliaji Wa Zamani Wa Bayern Munich Mwenye Umri Wa Miaka 68 Ameiambia
Televisheni Ya Sky Italia Kuwa Kocha Wa Manchester City Pep Guardiola Aliwasaidia
Katika Chaguo Lao. Kompany Ana Uzoefu Wa Bundesliga, Baada Ya Kuichezea Hamburg
Kabla Ya Kujiunga Na Man City.
Alichukua Mikoba Katika
Klabu Ya Burnley Mwaka Wa 2022, Na Kuwapandisha Katika Ligi Kuu Ya England Baada
Ya Kuibuka Mabingwa Wa Daraja La Pili Msimu Huo. Hata Hivyo, Klabu Hiyo
Ilishuka Daraja Baada Ya Msimu Mmoja Katika Ligi Ya Premier. Kompany Ndiye
Mgombea Wa Karibuni Kabisa Kwenye Orodha Ndefu Ya Makocha Waliohusishwa Na Bayern.