MAMIA Ya Watu Wamepoteza
Nafasi Zao Za Ajira Baada Ya Utawala Wa Kijeshi Nchini Guinea Kuvifungia Vituo
Vinne Vya Redio Na Viwili Vya Televisheni.
Hayo Yameelezwa Na
Muungano Wa Vyombo Vya Habari Ambao Unajiandaa Kuitisha Mgomo Wa Nchi Nzima.
Muungano Huo Siku Ya
Jumatatu Ulitishia Kuanzisha Mgomo Wa Nchi Nzima Usiokuwa Na Kikomo Baada Ya
Mamlaka Nchini Guinea Kufuta Leseni Za Uendeshaji Wa Shughuli Za Vituo Sita Vya
Habari Wakati Nchi Hiyo Ikiwa Inakabiliwa Na Wasiwasi Wa Kijamii Na Mazingira
Mabaya Ya Kisiasa.
Muungano Huo Wa Sppg Umevitaka Vyama Vyote Vya Wafanyakazi Kupitia
Barua Iliyoonekana Leo Na Afp, Kuunga Mkono Mgomo Huo.
Mamlaka Zimesema
Kufungiwa Vituo Hivyo Vya Habari
Kumetokana Na Vyombo Hivyo Kushindwa Kutekeleza Maagizo Kuhusu Maudhui
Wanayorusha Hewani.