FAMILIA Maskini Ambazo
Hazikupata Nafasi Ya Kuingia Katika Mpango Wa Kuwezesha Kaya Hizo Kupitia Mfuko
Wa Maendeleo Ya Jamii (Tasaf), Sasa Zitawezeshwa Pindi Awamu Mpya
Itakapotangazwa Na Serikali.
Tasaf Imesema Kila
Kinachofanyika Kinakwenda Kwa Utaratibu Na Kuzingatia Miongozo.
Ofisa Maendeleo Ya Jamii,
Nellusigwa Mwakigonja Amesema Hayo Hivi Karibuni, Wakati Akizungumza Na
Wananchi Wa Mohongay Wilayani Mbulu Katika Ziara Ya Watendaji Wa Tasaf Na Benki
Kuu Ya Dunia (WB).
“Tasaf Hii Ya Kunusuru
Kaya Maskini, Tulikuwa Na Awamu Ya Kwanza Iliisha Mwaka 2020, Tupo Awamu Ya
Pili Iliyopo Ukingoni, Tuwe Na Subira Inaweza Tukapata Fursa Kwenda Awamu Ya
Tatu Au Serikali Kuja Mpango Tofauti Utakaogusa Maisha Ya Wato," Amesema Mwakigonja.
“Mpango Huu Wa Tasaf
Umeanza Muda Mrefu Kidogo Na Ulikuwa Unakwenda Kwa Awamu Na Kaya Maskini Bado
Zinatakiwa Zifikiwe, Je Viongozi Wa Tasaf Na Benki Ya Dunia Mna Mpango Gani
Kuzisaidia Ili Kupata Unafuu Wa Maisha,” Amehoji Ibrahimu Dipobadi Mwanakijiji
Wa Mohongay.
Hata Hivyo, Katika Majibu
Yake Mwakigonja Amesema Serikali Inatambua Katika Kaya Za Watanzania Umaskini
Unaweza Kutokea Wakati Wowote, Hivyo Wakati Wa Awamu Ya Kwanza Baadhi Yao
Hawakuwa Na Sifa Za Kuingia Kwenye Mpango, Lakini Hivi Sasa Wana Vigezo.
“Tunatambua Mpango Huu,
Unatekelezwa Kwa Awamu, Kuna Watu Waliingia Mwaka 2015, Walitakiwa Kukaa Kwa
Miaka Mitatu Ili Kuwapisha Wengine, Lakini Baada Ya Utekelezaji Wa Miaka
Ilionekana Walengwa Bado Hawajanufaika Vema Hata Leo Hii Nani Yupo Tayari Kutoka.
“Lakini Wakati Tunaibua
Kaya Maskini, Mikutano Ilifanyika Kuna Kaya Zilikataa Wakidai Ni Freemason Na
Wengine Walisema Fedha Za Kampeni Leo Hii Wamegeuka Wanataka Kuingia Kwenye
Mchakato,” Amesema Mwakigonja.
Katika Ziara Hiyo
Wananchi Walihudhuria Mkutano Na Wawakilishi Wa Benki Ya Dunia Waliokwenda
Kukagua Shughuli Mbalimbali Za Utekelezaji Wa Miradi Ya Tasaf Inayolenga
Kuwasaidia Wananchi Kujikwamua Na Umaskini.
Mtaalamu Wa Mazingira
Tasaf, Amos Mkude Wa Tasaf Amesema Wameshirikiana Na WB Kuangalia Shughuli Za
Utekelezaji Wa Miradi Ya Tasaf, Ikiwamo Mafanikio Na Changamoto, Sambamba Na
Kushauri Namna Ya Kushauri Maeneo Yanayotakiwa Kuboreshwa Zaidi.
“Katika Mkoa Wa Manyara Tumetembelea
Vijijini Vinne Vya Wilaya Za Mbulu Na Hanang, Tumepata Nafasi Ya Kuzungumza Na
Watalaamu Wa Ngazi Ya Halmashauri,” Amesema Mkude.
Mbali Na Mkude, Mtaalamu
Mwingine Wa Mazingira Wa WB, Edina Kashangaki Amesema Amefurahishwa Na
Utekelezaji Wa Miradi Ya Tasaf Hasa Kwa Wananchi Kujiongeza Katika Shughuli Za
Kujiletea Maendeleo.
“Kuna Mzee Mmoja
Alituambia Kulikuwa Na Mpango Wa Kujenga Bwawa La Matumizi Ya Umma, Akachukua
Ujuzi Na Kuupeleka Shambani Kwake Kutengeneza Bwawa Dogo La Kumwagilia Miwa
Ambayo Ikistawi Anaweza Kupata Faida Ya Milioni Moja Hadi Mbili Baada Ya
Kuvuna,” Amesema.
Roselyn Kaihula Wa WB Amesema
Wanufaika Wanashukuru Miradi Ya Tasaf Kwa Sababu Inaboresha Maisha Licha Ya
Kupata Fedha, Wanapata Ujuzi Kupitia Miradi Inayotekeleza Katika Maeneo Yao.
“Kuna Maeneo Mengine Tabia
Za Wanakijiji Zimebadilika, Wengine Walikuwa Wanalewa, Wameacha Kutokana
Ushauri Wanaopewa Na Wataalamu Wa Tasaf Kuhusu Fedha. Ila Katika Vijiji Vingine
Kuna Kazi Kubwa Ya Kufanya Kutokana Na Utamaduni Tofauti,” Amesema Kaihula.