MARIAN ROBINSON, Mama yake Michelle Obama, Mkewe Rais Wa Zamani Wa Marekani Barack Obama Amefariki Dunia Akiwana Umri Wa Miaka 86.
Katika Taarifa Rasmi,
Familia Yake Imesema Kuwa Robinson Alifariki Ijumaa Asubuhi.
Robinson Alionekana Sana
Katika Ikulu Ya Marekani Katika Miaka Minane Ya Utawala Wa Barack Obama Kati Ya
Mwaka 2009 Hadi 2017.
Kwa Muda Mwingi Huo
Alishughulika Kuwalea Wajukuu Zake Wawili Malia Na Sasha – Binti Zake Michelle Na
Barack Obama.
Katika Taarifa Kwenye
Mtandao Wa X Uliofahamika Kama Twitter Zamani, Michelle Obama Alimueleza Mamake
Kuwa Kama Mtu Muhimu Kwake – "Jiwe La Singi Ambaye Siku Zote Alinisaidia
Kwa Chochote Nilichokihitaji".
" Alikuwa Kiungo
Muhimu Kwa Familia Yetu Yote Na Tumesikitika Kutangaza Kuwa Ameafiriki Dunia
Leo," Aliandika.
Katika Ujumbe Tofuati
Kwenye Mtandao Huo Wa X,Bwana Obama Amesema Kuwa“ Alikuwepo Na Atasalia Kuwepo Marian
Robinson Mmoja Pekee”.
“Katika Huzuni Wetu
Tunapata Nguvu Kwa Zawadi Ya Maisha Yake,” Aliongeza. “Na Kwa Maisha Yetu Yote
Tutajaribu Kuishi Kwa Mfano Wake.”
Hakuna Maelezo Zaidi
Yaliotolewa Kuhusu Chanzo Cha Kifo Chake.