JESHI LA SUDAN Limesema
Litajibu Vikali Shambulizi La Wanamgambo Wa RSF Katika Kijiji Cha Wad Al-Noura Siku
Ya Jumatano Ambalo Watetezi Wa Demokrasia Wanasema Liliwaua Zaidi Ya Watu 100.
Shambulizi Hilo Lilikuwa
Ni Kubwa Zaidi Katika Msururu Wa Mashambulizi Yaliyofanywa Na RSF Kwenye Vijiji
Vidogo Vidogo Kote Katika Jimbo La Gezira Linalosifika Kwa Kilimo, Baada Ya
Kuchukua Udhibiti Wa Mji Wake Mkuu Wa Wad Madani Mwezi Disemba.
Taarifa Ya Mkuu Wa Jeshi
Abdel Fattah Al-Burhan Inatolewa Baada Ya Madai Yaliyotolewa Na Wanaharakati Wa
Eneo Hilo Kwamba Jeshi Halikwenda Kuwasaidia Licha Ya Kuomba Msaada Siku Ya Jumatano.
Hata Hivyo Jeshi
Halikutaka Kuzungumzia Madai Hayo Hata Lilipoombwa Kufanya Hivyo. Afisa Wa
Ngazi Za Juu Wa Umoja Wa Mataifa Nchini Sudan Jana Alhamisi Alitoa Wito Wa
Uchunguzi Wa Shambulizi Hilo La Wad Al-Noura.
"Licha Ya Hali Mbaya
Katika Mzozo Wa Sudan, Lakini Picha Zinazoonyeshwa Kutoka Kwenye Eneo Hilo
Zinaumiza Sana," Alisema Mratibu Huyo Wa Masuala Ya Kiutu Clementine
Nkweta-Salami Kwenye Taarifa Yake.
Alikuwa Akizungumzia
Picha Zilizochapishwa Na Kamati Ya Watetezi Wa Demokrasia Huko Wad Madani Yaresistance
Committee Kwenye Mitandao Ya Kijamii, Ambayo Imekuwa Ikifuatilia Mashambulizi,
Zilizoonyesha Wahanga Waliokuwa Wamefunikwa Tayari Kwa Maziko.
Kulingana Na Kamati Hiyo,
Watu 104 Waliuawa Na Mamia Wengine Walijeruhiwa Katika Kijiji Hicho Cha Wad Al-Noura,
Na Sasa Wanamgambo Hao Wa RSF Wanaelekea Kwenye Vijiji Vingine.
Kundi Hilo Limewashutumu
Wanamgambo Hao Sio Tu Kwa Kuwashambulia Wanakijiji, Bali Pia Kupora Mali Zao Na
Kuwafanya Wanawake Na Watoto Kukimbilia Kwenye Mji Jirani Wa Managi Kuomba
Hifadhi. "Watu Wa Wad Al-Noura Waliomba Msaada Wa Jeshi, Lakini
Inasikitisha Kwa Sababu Hawakuja," Imesema Kamati Hiyo. "Haya Ni
Matukio Ya Kihalifu Yanayoakisi Tabia Ya Wapiganaji Kuwalenga Kwa Makusudi
Raia," Ilisema Sehemu Ya Taarifa Yao.
Shirika La Habari La Reuters
Lililoandika Taarifa Hii Halikuweza Kuwafikia Wakazi Ama Maafisa Wa Tiba Wa
Eneo Hilo Ili Kuthibitisha Taarifa Hizi Kutokana Na Kukatwa Kwa Mawasiliano Ya
Simu.
Wanamgambo Wa RSF Walianzisha
Mapigano Na Jeshi La Sudan Mwezi Aprili, 2023 Kufuatia Mzozo Baina Ya
Majenerali Wawili Wa Jeshi Na Tangu Hapo Wamechukua Udhibiti Wa Mji Mkuu Khartoum
Na Maeneo Mengi Ya Magharibi Mwa Sudan.
Na Sasa Wanataka Kusonga
Mbele Kuelekea Katikati Mwa Sudan, Wakati Umoja Wa Mashirika Ya Umoja Wa Mataifa
Yakisema Watu Wa Taifa Hilo Wanakabiliwa Na Kitisho Kikubwa Cha Njaa.