WAZIRI MKUU Wa Israel
Benjamin Netanyahu Atahutubia Wabunge Wa Marekani Mjini Washington DC Tarehe 24
Julai, Viongozi Wa Bunge Walitangaza Alhamisi.
Atazungumza Na Mabaraza
Yote Mawili Ya Congress - Seneti Na Baraza La Wawakilishi - Wakati Vita Vya Israel
Na Gaza Vikiendelea.
Republican Na Democrats Wote
Walimwalika Waziri Mkuu Kuzungumza, Lakini Tarehe Ya Hotuba Yake Haikuwekwa
Rasmi Hadi Alhamisi.
Mwezi Uliopita Mwendesha
Mashtaka Wa Mahakama Ya Kimataifa Ya Jinai Aliomba Hati Ya Kukamatwa Kwa
Kiongozi Huyo Wa Israel Na Waziri Wake Wa Ulinzi, Yoav Galant, Kwa Tuhuma
Zinazohusiana Na Vita.
Bw Netanyahu Alilaani
Hatua Ya ICC, Akisema Alikataa Kwa Kuchukizwa Na Kwamba "Israel Ya
Kidemokrasia" Imelinganishwa Na Kile Alichokiita "Wauaji Wa
Halaiki".
Bw Netanyahu Alisema,
Kulingana Na Taarifa Iliyotolewa Na Viongozi Wa Bunge, Kwamba "Ameguswa
Sana Kupata Fursa Ya Kuiwakilisha Israel... Kuwasilisha Ukweli Kuhusu Vita
Vyetu Vya Haki Dhidi Ya Wale Wanaotaka Kutuangamiza".
Katika Barua Yao Ya
Kumwalika Waziri Mkuu, Spika Wa Bunge Mike Johnson Na Kiongozi Wa Wachache Katika
Seneti Mitch Mcconnell - Wote Wakiwa Warepublican - Walisema Wanatumai Bw
Netanyahu Angechukua Fursa Hiyo "Kushirikisha Maono Ya Serikali Ya Israel Ya
Kutetea Demokrasia, Kupambana Na Ugaidi, Na Kuanzisha Haki Na Amani Ya Kudumu
Katika Eneo Hilo".
Ziara Ya Bw Netanyahu Inajiri
Huku Uhusiano Wake Na Marekani Ukizidi Kuwa Wa Wasiwasi, Hasa Miongoni Mwa
Viongozi Wakuu Wa Chama Cha Democrats Nchini Marekani.