MAREKANI imesema
itapeleka msaada wa kijeshi wa karibu dola milioni 225 nchini Ukraine katika
kifurushi kipya kinachojumuisha risasi.
Msaada huo mpya unatolewa
wakati Rais Joe Biden akisisitiza tena kwamba wataendelea kuisaidia Ukraine na
kamwe hawataruhusu Urusi kuitisha Ulaya.
Silaha hizo zitakatumiwa
na vikosi vya Kyiv kushambulia ndani ya Urusi ili kuulinda mji wake wa Kharkiv unaoshambuliwa
vikali na Urusi.
Alitoa hakikisho hilo
katika hotuba ya jana Alhamisi mbele ya kaburi la Wamarekani kwenye eneo la
Normandy wakati wa kumbukumbu ya miaka 80 ya D-Day.
Marekani hivi karibuni
iliipa idhini Ukraine kutumia silaha zake kushambulia ndani ya Urusi na hii leo
Biden anatarajiwa kukutana na Rais Volodymyr Zelensky mjini Paris.