CHELSEA wamemfanya winga
wa Crystal Palace na Ufaransa aliye katika kikosi cha chini ya umri wa miaka 21
Michael Olise, 22, kuwa mmoja wa walengwa wao wakuu wa uhamisho wa majira ya joto,
huku The Blues wakiwa tayari kupambana na Manchester United ili kumnasa
mchezaji huyo anayekadiriwa kuwa na thamani ya pauni milioni 60. (Standard)
Mshambulizi wa Chelsea
Romelu Lukaku yuko tayari kuhama huku klabu nyingi zikiwa na nia ya kumtaka,
Dominic Calvert-Lewin anaweza kuondoka Everton kwa uhamisho wa bure na
Manchester United wamewasilisha ombi la kumnunua mlinzi chipukizi.
Mshambulizi wa Chelsea na
Ubelgiji Romelu Lukaku, 31, amefungua milango ya kuhamia Saudi Pro League
lakini pia anazivutia AC Milan, Napoli na kutoka kwa Jose Mourinho kwa ajili ya
kuungana tena na meneja wake wa zamani katika klabu ya Fenerbahce. (Telegraph,
usajili unahitajika)
Uhamisho wowote wa Napoli
kwa Lukaku utatokea tu ikiwa watafanikiwa kumuuza mshambuliaji wa Nigeria
Victor Osimhen, 25, kwanza. (Times, usajili unahitajika)
Manchester United
wamewasilisha ombi la euro 60m kumnunua mlinzi wa Lille Leny Yoro, 18, lakini
wanakabiliwa na ushindani wa kuwania saini ya kinda huyo wa Ufaransa na Real
Madrid. (Marca kwa Kihispania)
Borussia Dortmund
wanataka kumsajili beki wa kushoto wa Uholanzi Ian Maatsen, 22, kwa mkataba wa
kudumu baada ya kuonyesha kiwango kizuri akiwa kwa mkopo lakini wanasita
kufikia thamani ya Chelsea ya pauni milioni 35. (ESPN)
Everton wana hatari ya
kumpoteza mshambuliaji wa Uingereza Dominic Calvert-Lewin kwa uhamisho wa bila
malipo mwaka 2025 baada ya kusitishwa kwa mazungumzo ya kandarasi na mchezaji
huyo mwenye umri wa miaka 27. (Football Insider)
Sheffield United
wameonyesha nia yao ya kutaka kumsajili beki wa Nottingham Forest Muingereza
Joe Worrall, huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 akipatikana kwa
uhamisho wa bure mkataba wake utakapokamilika msimu wa joto. (Football Insider)
Kiungo wa kati wa Chelsea
na England Conor Gallagher, 24, yuko tayari kusalia katika klabu hiyo licha ya
Aston Villa na Tottenham kumtaka. (Guardian)
Vilabu sita vya Ligi ya
Premia - Chelsea, Aston Villa, Newcastle, Everton, Nottingham Forest na
Leicester - vinakabiliwa na kulazimika kuuza wachezaji kabla ya mwisho wa Juni
ili kuzingatia Sheria za Faida na Uendelevu (Sky Sports)
Mshambulizi wa England na
Bournemouth Dominic Solanke, 27, ana kipengele cha kuachiliwa huru cha £65m
katika kandarasi yake, lakini kinaweza tu kutumika na vilabu fulani. (Athletic,
usajili unahitajika)
Brighton wamemuweka
Fabian Hurzeler mwenye umri wa miaka 31 kwenye orodha yao meneja ajaye. Kocha
huyo mzaliwa wa Marekani aliiongoza St Pauli kupanda daraja kutoka Bundesliga 2
msimu uliopita. (Telegraph, usajili unahitajika)
Brighton wamefanya
mazungumzo na bosi wa zamani Graham Potter, 49, kuhusu uwezekano wa kurejea
kama meneja.(Guardian)
Mlinzi wa kati wa Arsenal
na Brazil Gabriel, 26, alisema ni "ndoto yake" kujiunga na klabu ya
Corinthians ya Brazil, timu ambayo amekuwa akiiunga mkono tangu akiwa
mtoto(Mirror)
Newcastle United wapo
kwenye mazungumzo ya hali ya juu na beki wa Bournemouth Lloyd Kelly, huku West
Ham, Tottenham, Roma na Atletico Madrid pia wakimtaka Mwingereza huyo mwenye
umri wa miaka 25, ambaye atapatikana kwa uhamisho wa bure(Chronicle)