MATOKEO rasmi ya uchaguzi
mkuu Afrika kusini yanatarajiwa kutangazwa Jumapili jioni, afisa mmoja wa tume
anasema.
Zoezi la kuhesabu kura
linaingia katika hatua ya mwisho huku 98% ya matokeo yakiwa yamepokewa tayari.
Naibu mkurugenzi mtendaji
wa tume ya uchaguzi nchini Mawethu Mosery, ameiambia televisheni ya eNCA kwamba
tume itakesha usiku kucha Jumamosi kukabiliana na pingamizi na maombi.
Chama tawala ANC
kinatarajiwa kupoteza nguvu kilichoshikilia katika miongo mitatu ya siasa baada
ya kupungua kwa wafuasi wake kwa kiwango kikubwa.
Tags
POLITICS