WIZARA Ya Uchukuzi Ya Japan
Ilivamia Makao Makuu Ya Kampuni Kubwa Ya Magari Ya Toyota Siku Ya Jumanne, Huku
Kashfa Kuhusu Data Mbovu Ya Usalama Ikiongezeka.
Mtengenezaji Mkuu Wa
Magari Duniani Ameomba Radhi Kwa Kutoa Data Isiyo Sahihi Au Iliyodanganywa Kwa
Ajili Ya Majaribio Ya Vyeti Vya Usalama.
Kashfa Hiyo Imetikisa
Sekta Ya Magari Ya Japan, Huku Wapinzani Wao Honda, Mazda Na Suzuki Pia
Wakikiri Kuwasilisha Data Mbovu.
Toyota Iliuza Zaidi Ya
Magari Milioni 11 Ya Abiria Mnamo 2023.
Imesema Matokeo Hayo
Hayaathiri Usalama Wa Magari Ambayo Tayari Yapo Barabarani.
Kampuni Hiyo Imesitisha
Utengenezaji Wa Aina Tatu Za Magari - Corolla Fielder, Corolla Axio Na Yaris
Cross.
Pia Imeshutumiwa Kwa
Kutumia Magari Yaliyorekebishwa Wakati Wa Majaribio Ya Mgongano Wa Usalama, Kwa
Magari Ambayo Hayatengenezwi Tena.
Uvamizi Huo Umefanyika
Siku Moja Baada Ya Mwenyekiti Wa Toyota Akio Toyoda Kuomba Msamaha Kwa Wateja
Na Wapenzi Wa Magari Yao.
Aliinamisha Kichwa Sana
Na Kukaa Hivyo Kwa Sekunde Chache, Jambo Ambalo Ni Kawaida Nchini Japani Wakati
Kampuni Zinaomba Msamaha Kwa Makosa Waliofanya.
"Tulipuuza Mchakato
Wa Uidhinishaji Na Kwa Wingi Tukazalisha Magari Yetu Bila Kwanza Kuchukua Hatua
Zinazofaa Za Tahadhari," Bw Toyoda Alisema.