CHAMA AKABIDHIWA RASMI JEZI YAKE YANGA


KIUNGO Mpya Wa Yanga, Clatous Chama, Amekabidhiwa Jezi Namba 17 Ndani Ya Timu Hiyo, Ambayo Wengi Walizoea Kumuona Akiitumia Wakati Akiwa Simba.


Chama, Mara Baada Ya Kutua Yanga, Alilazimika Kutumia Jezi Namba 20 Iliyokuwa Ikivaliwa Na Zawadi Mauya Ambaye Alitemwa.


Hata Hivyo Baada Ya Mazungumzo Na Winga Farid Mussa, Aliyekuwa Anaitumia Jezi Namba 17, Amekubali Kumpa Chama Jezi Hiyo.

Mapema Farid, Alionyesha Hana Kinyongo Kwa Kumuachia Chama Namba Hiyo, Endapo Atahitaji Kumuachia.

Kwa Maamuzi Hayo Sasa Farid Ambaye Ameongeza Mkataba Wa Kuendelea Kuitumikia Yanga, Atakuwa Anaitumia Jezi Namba 12 Aliyochagua.

Kuonyesha Maridhiano Hayo Farid Mwenyewe Amemkabidhi Chama Jezi Hiyo Wakiwa Wameishika Pamoja Na Kupeana Mikono.

Akiwa Simba Chama Kwa Miaka Mingi Amekuwa Akitumia Jezi Hiyo Namba 17 Ambapo Hata Alipoondoka Na Kurejea Alirudishiwa Na Kuendelea Kuitumia.

Kiungo Huyo Amejiunga Na Yanga Akitokea Simba Kwa Mkata Wa Mwaka Mmoja Baada Ya Kumaliza Kandarasi Yake Msimbazi.

JISAJIRI SASA NA PLAY MASTER BET - BETI KIRAHISI

BONYEZA HAPA KUJISAJIRI


Previous Post Next Post

ADVERT

ADVERT