MAHAKAMA Ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar Es Salaam, Imeamuru Uongozi Wa
Club Ya Yanga Ukiongozwa Na Rais Wa Yanga Injinia Hersi Saidi Na Wenzake,
Kuachia Ngazi Na Kuondoka Kwenye Club Hiyo Kwakuwa Katiba Ya Yanga Haitambui
Uwepo Wao.
Imedaiwa Kuwa Uamuzi Huu Wa Mahakama Umekuja
Baada Ya Kundi La Wazee Wachache Waliowahi Kuwa Wazee Wa Yanga Kipindi Cha
Nyuma, Kushitaki Mahakamani Likidai Uwepo Wa Viongozi Wa Sasa Wa Yanga (Injinia
Hersi Na Wenzake) Ni Batili Na Haujafuata Katiba Ya Club Hiyo.
Kutokana Na Wazee Hao Kushinda Kesi Hiyo Katika Mahakama
Ya Hakimu Mkazi Kisutu, Inamaana Kuwa Rais Wa Yanga Injinia Hersi Na Viongozi Wenzake
Wanatakiwa Kuachia Ngazi Na Kukabidhi Ofisi Kuanzia Sasa.
Injinia Hersi Alianza Kuiongoza Yanga Kama Rais Miaka
Miwili Iliyopita Baada Ya Kushinda Nafasi Hiyo Akiwa Ni Mgombea Pekee July 2022
Na Kumfanya Kuwa Rais Wa Kwanza Wa Yanga SC Toka Kuanza Kwa Mfumo Mpya Wa
Mabadiliko Ambapo Alitangazwa Kuwa Atakuwa Madarakani Kwa Miaka Minne ( Hadi
2026 ) Kwa Mujibu Wa Katiba Ya Club Hiyo.
JISAJIRI
SASA NA PLAY MASTER BET - BETI KIRAHISI
BONYEZA
HAPA KUJISAJIRI