Mahakama Ya Kijeshi Nchini Kongo Imewahukumu
Adhabu Ya Kifo Watu 37, Wakiwemo Wamarekani Watatu, Baada Ya Kuwatia Hatiani
Kwa Mashtaka Ya Kushirki Katika Jaribio La Mapinduzi.
Washtakiwa Hao, Wengi Wao Wakiwa Raia Wa Kongo,
Lakini Wakiwemo Pia Muingereza, Mbelgiji Na Mcanada, Wana Muda Wa Siku Tano
Kukata Rufaa Dhidi Ya Hukumu Hiyo, Inayohusisha Pia Mashtaka Ya Ugaidi Na
Ushirika Wa Uhalifu.
Watu 14 Wameachiwa Huru Katika Kesi Hiyo
Iliyoanza Mwezi Juni. Watu Sita Waliuawa Wakati Wa Jaribio Hilo Lililoongonzwa
Na Mpinzani Asiemaarufu Christian Malanga Mnamo Mwezi Mei, Ambalo Lililenga
Kasri La Rais Na Mshirika Wa Karibu Wa Rais Felix Tshisekedi.
Malaga Aliuawa Katika Ufyatulianaji Risasi Na Vikosi Vya Usalama Vilipojaribu Kumkamata, Na Mtoto Wake Marcel Malanga, Ambaye Ni Raia Wa Marekani Mwenye Umri Wa Miaka 21 Ni Miongoni Mwa Waliohukumiwa Kifo.
JISAJIRI SASA NA PLAY MASTER BET - BETI KIRAHISI
BONYEZA HAPA KUJISAJIRI