MFANYABIASHARA Bilionea
Wa Mali Isiyohamishika Wa Marekani Na Tajiri Na Msafiri Wa Ohio Larry Connor, Patrick
Lahey, Mwanzilishi Mwenza Wa Manowari Ya Triton, Wanasema Wanataka Kusafiri
Chini Ya Bahari Hadi Kina Cha Karibu 3,800m (12,467ft) Ili Kuona Ajali Ya Meli
Ya Titanic Katika Bahari Ya Atlantiki Kaskazini.
Sekta Ya Kibinafsi Ya
Safari Ya Chini Ya Maji Ilitikisika Baada Ya Watu Watano Kupoteza Maisha Wakati
Meli Iliyojengwa Na Oceangate Ilipokwama Ilipokuwa Ikielekea Titanic Mwaka
Jana.
Msemaji Wa Kampuni Ya Bw.Connor
Alisema Jumanne Kwamba Safari Iliyopendekezwa Itafanyika Mara Tu Chombo
Kitakapoidhinishwa Kikamilifu Na Shirika La Wanamaji.
Hakuna Muda Uliopangwa Wa
Safari. Wawili Hao Wanapanga Kutumia Manuwari Ndogo Inayoitwa Triton 4000/2 Abyssal
Explorer - "4000" Kinachoweza Kwenda Kina Cha Umbali Ambao Chombo
Kinaweza Kwenda Kwa Usalama.
Manowari Ya Titan Iliyojengwa
Na Oceangate Ilitengenezwa Kwa Nyuzinyuzi Za Kaboni Na Iliidhinishwa Tu Hadi
Mita 1,300, Kina Fupi Sana Cha Sakafu Ya Bahari Ambapo Mabaki Ya Meli Ya Titanic
Yapo.