KLABU
Kadhaa Za Ligi Kuu Ya Saudia (Saudi Pro), Ikiwemo Al Nassr, Al Ahli Na Al
Qasidiya, Zinawania Kumsajili Kiungo Wa Kati Wa Timu Ya Taifa Ya Brazil
Casemiro, 32, Kutoka Manchester United Msimu Huu. (Goal - Kwa Kireno)
Barcelona
Huenda Wakamrejesha Nou Camp Kwa Mara Ya Pili Mshambuliaji Wa Ureno Joao Felix Kutoka
Atletico Madrid. (Sport - Kwa Kihispania)
Liverpool
Wameweka Thamani Ya Pauni Milioni 20 Kwa Mlinzi Wa Uholanzi Sepp Van Den Berg,
22, Ambaye Ananyatiwa Na Klabu Za Brentford, Southampton Na Wolfsburg Baada Ya
Kung'aa Alipokuwa Mainz Kwa Mkopo. (Athletic, Usajili Unahitajika)
Kinyang'anyiro
Cha Kumsaka Mshambuliaji Wa RB Leipzig Na Uhispania Dani Olmo Kimeshika Kasi,
Huku Barcelona, Manchester United, Manchester City, Liverpool Na Bayern
Munich Zikimtaka Mchezaji Huyo Mwenye Umri Wa Miaka 26. (Mundo Deportivo - Kwa Kihispania)
Southampton
Wanawania Saini Ya Winga Wa Sunderland Muingereza Jack Clarke, 23. (Telegraph -
Usajili Unahitajika)
Inter
Milan Wanavutiwa Na Beki Mwingereza Aaron Wan-Bissaka, 26, Ambaye Manchester
United Imeweka Thamani Yake Kuwa Euro 12m (£10.2m). (Tuttomercatoweb - Kwa Kiitaliano)
Napoli
Hawana Nia Ya Kumuuza Winga Wa Georgia Khvicha Kvaratskhelia, 23, Kwa Paris St-Germain,
Huku Antonio Conte Akitarajiwa Kuwa Kocha Wao Mkuu Mpya. (Corriere Dello Sport Kwa
Kiitaliano)
Arsenal
Na Kocha Mikel Arteta Wapo Kwenye Mazungumzo Kuhusu Mkataba Mpya Wa Kudumu
Katika Klabu Hiyo. (Football Insider)
Nia
Ya Xavi Ya Kumuuza Mshambuliaji Wa Poland Robert Lewandowski Mwenye Umri Wa
Miaka 35 Msimu Huu Ilikuwa Sababu Kuu Ya Mhispania Huyo Kufukuzwa Kazi Barcelona
Mwezi Huu. (Sport - Kwa Kihispania)
Mshambuliaji
Wa Real Madrid Wa Brazil Rodrygo, 23, Ametilia Shaka Mustakabali Wake Katika
Klabu Hiyo, Na Hivyo Kuongeza Uwezekano Wa Kuhamia Liverpool. (Mundo Deportivo -
Kwa Kihispania, Kupitia Dazn)
Newcastle
Wanashinikiza Kupata Jibu Kuhusu Uwezekano Wa Kumnunua Beki Wa Uingereza Tosin
Adarabioyo, Huku Mchezaji Huyo Mwenye Umri Wa Miaka 26 Akitarajiwa Kuondoka Fulham
Msimu Huu Wa Joto Mkataba Wake Utakapomalizika. (Talksport)
West
Ham Wamefikia Mkataba Wa Pauni Milioni 15 Na Flamengo Kumnunua Mlinzi Wa Brazil
Fabricio Bruno, 28. (Guardian)
Aston
Villa Na Crystal Palace Wanatazamia Kumnunua Beki Wa Gent Muingereza Archie
Brown, 22. (Mirror)
Mshambuliaji
Wa Manchester United Muingereza Mason Greenwood Anataka Kurejea Katika Klabu Ya
Getafe Ya Uhispania Msimu Ujao Baada Ya Mchezaji Huyo Mwenye Umri Wa Miaka 22
Hivi Majuzi Kucheza Mechi Yake Ya Mwisho Kama Mchezaji Wa Mkopo Katika Klabu
Hiyo Ya La Liga. (Teamtalk)