MAWAKILI Wa Donald Trump Na
Waendesha Mashitaka Wa Manhattan Wametoa Hoja Zao Za Mwisho Jana Kwa Jopo La
Watoa Uamuzi Wa Mahakama. Hukumu Ya Kesi Hiyo Itakuwa Na Umuhimu Mkubwa Kwa Trump
Na Taifa La Marekani.
Mwendesha Mashitaka Joshua
Steinglass Amewaambia Watoa Uamuzi, Kuwa Trump Alishiriki Katika Njama Ya
Kuwalaghai Wapiga Kura Katika Mwaka Wa 2016.
Kesi Hiyo Ya Kihistoria,
Inahusu Madai Kuwa Trump Na Washirika Wake Walikula Njama Ya Kuficha Habari Za
Kuwaaibisha Wakati Wa Kampeni Za Uchaguzi Wa Mwaka Wa 2016 Kwa Kuwalipa Watu
Akiwemo Mcheza Filamu Za Ngono Aliyedai Kuwa Yeye Na Trump Walifanya Mapenzi
Muongo Mmoja Uliotangulia.
Naye Wakili Wa Trump Todd
Blanche Alisema Hakuna Yeyote Kati Ya Mchezafilamu Huyo, Stormy Daniels Wala
Mwanasheria Wa Trump Aliyemlipa Mwanamke Huyo, Michael Cohen, Anayeweza
Kuaminiwa.
Amesema Rais Trump Hana
Hatia, Kwa Sababu Hakufanya Uhalifu Wowote, Na Mwendesha Mashitaka Hakuweza
Kuthibitisha Kikamilifu Mashitaka Hayo. Ikiwa Ni Chini Ya Miezi Sita Kabla Ya
Uchaguzi Ambao Trump Anatafuta Kurejea Katika Ikulu Ya White House, Umuhimu Wa
Hukumu Ya Kesi Hiyo Ni Mkubwa Kwa Trump Mwenye Umri Wa Miaka 77 Na Kwa Marekani.