TAKRIBANI Watu 15
Wamepoteza Maisha Wakati Kimbunga Na Dhoruba Zilipokumba Maeneo Ya Kati Ya Marekani,
Na Kuharibu Nyumba Na Kukata Umeme Kwenye Makazi Ya Mamia Kwa Maelfu Ya Watu.
Watu Saba Walipoteza
Maisha Kaskazini Mwa Texas, Watano Huko Arkansas, Wawili Huko Oklahoma Na Mmoja
Huko Kentucky.
Wengine Wengi
Walijeruhiwa, Na Karibu 500,000 Hawakuwa Na Umeme Katika Majimbo Kadhaa Siku Ya
Jumapili.
Gavana Wa Texas Greg
Abbott Alisema Zaidi Ya Theluthi Moja Ya Kaunti Zote Katika Jimbo Lake Sasa
Zinakabiliwa Na Tangazo La Maafa.
Sheriff Ray Sappington Wa
Kaunti Ya Cook, Texas, Alisema Idadi Ya Waliofariki Hapo Ni Pamoja Na Watoto
Wawili Wenye Umri Wa Miaka Miwili Na Mitano Na Watu Watatu Wa Familia Moja.
"Ni Uchafu Sasa
Uliosalia," Alisema Sheriff Wa Eneo La Valley View, Ambalo Lilikuwa
Miongoni Mwa Yale Yaliyoathiriwa Zaidi Na Kimbunga Kikali.
Radi, Ngurumo Na Mvua
Kubwa Wakati Huo Huo Zililazimisha Kuhamishwa Kwa Watu Wapatao 125,000 Huku
Mbio Za Jumapili Za Indianapolis 500 Zikiahirishwa Kwa Saa Nne.