SHERIA Hiyo Ya Msingi
Ilianza Kutumika Tarehe 23 Mwezi Mei Mwaka 1949, Ambayo Pia Ni Tarehe Ya
Kuanzishwa Kwa Shirikisho La Ujerumani Miaka 35 Iliyopita. Rais Frank Walter
Steinmeier Amesema Zawadi Hiyo Kuu Kwa Ujerumani Haipaswi Tu Kukumbukwa,
Inatakiwa Kuenziwa, Kutunzwa Na Kulindwa Kila Siku Nchini Ujerumani. Amesema Katiba
Hiyo Imeunda Mfumo Thabiti Unaoleta Muingiliano Wa Amani Wa Watu Katika Jamii
Mbali Mbali.
Akiwa Katika Maadhimisho
Ya Miaka Hiyo 75 Ya Katiba Ya Ujerumani Au Sheria Mama, Steinmeier Amesema
Katiba Hiyo Ni Moja Ya Katiba Kongwe Ujerumani Na Imekuwa Mfano Kwa Katiba
Nyengine Nyingi. Kiongozi Huyo Wa Ujerumani Amesema Sheria Hiyo Kuu
Inayoiongoza Nchi Hadi Sasa Ndio Imekuwa Msingi Wa Uhuru, Demokrasia Na Haki Na
Kuhakikisha Utangamano Wa Watu Wa Ujerumani.
Kwa Maoni Yake Katiba
Iliyoundwa Miaka 75 Iliyopita Ni Imara Na Imeivusha Nchi Katika Migogoro Kadhaa
Pamoja Na Changamoto Chungu Nzima.
Kando Na Hayo Steinmeier Ametahadharisha
Kwamba Mashambulizi Ya Kisiasa Yameanza Kushuhudiwa Tena Nchini Ujerumani Akisema
Ana Wasiwasi Juu Ya Ongezelo La Mashambulizi Dhidi Ya Wanasiasa Wanaokuwa
Kazini Au Katika Kampeni Mbali Mbali. Ameongeza Kuwa Vurugu Zinahatarisha
Demokrasia Ya Nchi Na Kusambaratisha Misingi Yake.
Rais Steinmeier Wa Ujerumani,
Sasa Amewatolea Mwito Wajerumani Wote Kudumisha Utamaduni Wa Kisiasa
Inayoendana Na Na Demokrasia.
Sherehe Ya Kuadhimisha
Miaka Hiyo Imehudhuriwa Na Viongozi Watano Wa Vyombo Vya Katiba. Kando Na Rais
Mwenyewe Alikuwepo Pia Rais Wa Bunge La Ujerumani Bundestag Bärbel Bas, Rais Wa
Baraza La Juu La Bunge La Ujerumani, Manuela Schwesig, Rais Wa Mahakama Ya
Katiba Stephan Harbarth Pamoja Na Kansela Wa Ujerumani Olaf Scholz.
Baadae Wananchi Pia
Watakuwa Na Nafasi Ya Kusherehekea Katiba Yao Katika Hafla Ya Demokrasia
Itakayoandaliwa Katika Majengo Ya Serikali Ya Mjini Berlin Kuanzia Kesho Ijumaa
Hadi Jumapili Na Siku Ya Jumamosi Katika Majengo Ya Serikali Za Wilaya Mjini Bonn
Ambapo Rais Frank-Walter Steimeier Anatarajiwa Kufungua Makaazi Yake Mapya
Mjini Humo Yaliyopewa Jina La Hammerschmidt.