RAIS Emmanuel Macron Wa Ufaransa
Ameupongeza Ushirikiano Wa Muda Mrefu Wa Nchi Yake Na Ujerumani, Wakati Akianza
Ziara Yake Ya Kiserikali Ya Siku Tatu Mjini Berlin Inayolenga Kudhihirisha
Nguvu Ya Uhusiano Huo.
Ziara Ya Kiserikali Ya Macron
Nchini Ujerumani, Ya Kwanza Kufanywa Na Rais Wa Ufaransa Katika Miaka 24,
Inajiri Wakati Madola Hayo Mawili Makubwa Ulaya Yanakabiliwa Na Matatizo
Mbalimbali, Kuanzia Vita Vinavyorindima Kwenye Mlango Wa Umoja Wa Ulaya Nchini Ukraine
Mpaka Kuongezeka Kwa Vyama Vya Siasa Kali Za Mrengo Wa Kulia Katika Umoja Huo
Na Uwezekano Wa Kurejea Madarakani Donald Trump Mjini Washington.
Macron Amesema Ulaya Ipo
Katika Wakati Muhimu Wa Maamuzi, Akitaja Uvamizi Wa Kijeshi Wa Urusi Pamoja Na
Changamoto Zinazohusiana Na Mabadiliko Ya Tabianchi Na Akili Ya Kubuni - AI.
Amesema Ili
Kuyashughulikia Masuala Hayo, Ushirikiano Kati Ya Ufaransa Na Ujerumani Unahitajika.
Katika Kikao Cha Waandishi Habari Pamoja Na Rais Wa Ujerumani Frank Walter-Steinmeier
Katika Ikulu Ya Bellevue Mjini Berlin, Macron Alisema Ushirikiano Kati Ya Ujerumani
Na Ufaransa Ni Kama Wanandoa Wachangamfu, Wenye Masharti Na Malengo Makubwa.
Steinmeier Ameiitaziara
Ya Macronkuwa Ni Uthibitisho Wa Ukubwa Wa Urafiki Kati Ya Ufaransa Na Ujerumani.
Macron Aliwasili Jana Berlin Na Akashiriki Tamasha La Demokrasia Lililoadhimisha
Miaka 75 Ya Katiba Ya Ujerumani Iliyoanza Kutumika Katika Iliyokuwa Ujerumani Ya
Magharibi Baada Ya Vita Vya Pili Vikuu Vya Dunia.
Kisha Baadae Akaandaliwa
Dhifa Ya Chakula Cha Jioni Iliyohuhudhuriwa Na Wanasiasa Wakuu, Akiwemo Kansela
Olaf Scholz.
Ziara Ya Macron Imejiri
Kabla Ya Uchaguzi Wa Ulaya Utakaoamua Bunge Lijalo La Ulaya. Vyama Vya Siasa
Kali Za Mrengo Wa Kulia Katika Umoja Wa Ulaya Vimehuhudia Ongezeko La Uungwaji
Mkono Katika Miaka Ya Karibuni – Ikiwemo Ufaransa Na Ujerumani – Na
Vinatarajiwa Kufanya Vyema Katika Uchaguzi Huo Wa Juni 6 – 9.
Uhusiano Kati Ya Paris Na
Berlin Kwa Muda Mrefu Umeonekana Kuwa Nguvu Inayoendesha Ulaya, Kisiasa Na
Kiuchumi. Lakini Msuguano Ulianza Kuzuka 2022, Baada Ya Angela Merkel Kuondoka
Jukwaa La Kisiasa La Ujerumani, Ijapokuwa Macron Na Scholz Katiku Ziku Za
Karibuni Wamefanya Juhudi Za Kuimarisha Ushirikiano.
Makubaliano Yamepatikana
Kuhusu Masuala Kadhaa, Ikiwemo Mageuzi Ya Sheria Za Umoja Wa Ulaya Za Madeni Na
Nakisi, Lakini Mambo Mengine Ya Mgongano Bado Yapo, Hasa Kiwango Cha Msaada Wa
Kijeshi Kwa Ukraine Na Majibu Ya Kiuchumi Ya Umoja Wa Ulaya Kwa Hatua Za Ulinzi
Wa Masoko Za China Na Marekani. Maswali Hayo Nyeti Na Mengine Yanatarajiwa
Kujadiliwa Katika Mkutano Wa Mawaziri Wa Ufaransa Na Ujerumani Jumanne. Jumatatu
Macron Na Mkewe Watakwenda Dresden. Atatoa Hotuba Kuhusu Sera Ya Ulaya.
Jumanne, Watakuwa Mjini Münster,
Ambako Macron Atapewa Tuzo Ya Amani Ya Westphalia. Macron Aliingia Madarakani Ufaransa
Miaka Saba Iliyopita Na Hawezi Kugombea Kwa Muhula Wa Tatu Katika Uchaguzi Ujao
Wa Rais Mwaka Wa 2027.