RAIS Wa Mpito Wa Burkina
Faso, Kapteni Ibrahim Traore Anatarajiwa Kubakia Madarakani Kwa Kipindi Cha
Miaka Mitano Kuanzia Julai 2, 2024 Hadi 2029.
Uamuzi Huo Umekuja Baada
Ya Kufanyika Mashauriano Ya Kitaifa Jumamosi, Mei 25, Yaliyojumuisha Mashirika
Ya Kiraia, Vikosi Vya Usalama Na Wabunge Wa Mpito Huku Vyama Vya Kisiasa
Vikiachwa Kando.
"Muda Wa Mpito
Umepangwa Kuwa Miezi 60 Kutoka Julai 2, 2024," Alisema Kanali Moussa
Diallo, Aliyekuwa Mwenyekiti Wa Kamati Ya Mazungumzo Hayio Ya Kitaifa Katika
Hotuba Yake.
Burkina Faso Ni Moja Ya
Ya Nchi Za Afrika Magharibi Ambazo Jeshi Limechukua Madaraka, Likizishutumu Serikali
Zilizochaguliwa Kwa Kushindwa Kutimiza Ahadi Zake.
Traore Aliongoza
Mapinduzi Hayo Ya Kijeshi Septemba 2022 Kwa Kuuondoa Utawala Wa Kijeshi Wa Luteni
Kanali Paul Damiba, Takriban Miezi Minane Baada Ya Kufanya Mapinduzi Ya
Kumuondoa Rais Aliyechaguliwa Kidemokrasia Roch Marc Kaboré.