MAKAMU Wa Rais Wa Jamhuri
Ya Kenya, Mheshimiwa Rigathi Gachagua Amesema, Ana Uhusiano Mzuri Wa Kikazi Na Rais
Dkt.William Ruto.
Pia, Amesema Kuwa Rais
Dkt.Ruto Amempa Majukumu Ya Kutosha Kuondoa Uvumi Kwamba Uhusiano Wao Unayumba.
Mheshimiwa Righati
Gachagua Ambaye Siku Chache Zilizopita Aliwakashifu Baadhi Ya Wanasiasa Wa Rift
Valley Kwa Kuingilia Siasa Za Mlima Kenya Alitaja Uhusiano Wake Na Rais Dkt.Ruto
Kama Uhusiano Wa Hali Ya Juu Unaolenga Kuimarisha Amani Na Umoja Kote Nchini.
“Mimi Na Rais Ruto Tuko
Katika Uhusiano Mzuri, Kwa Kweli Rais Amenipa Majukumu Mengi Kama Naibu Wake Na
Lengo Letu Kwa Sasa Ni Kuwaunganisha Wakenya Wote Hasa Wale Ambao Waliingiliwa
Na Hofu Wakati Wa Uchaguzi Mkuu Uliopita,” Amesema Gachagua.
Akizungumza Mwishoni Mwa
Wiki Katika Shule Ya Msingi Ya Matharu Katika Kaunti Ya Uasin Gishu Wakati Wa
Kuchangisha Fedha Za Kusaidia Makanisa 15 Kutoka Eneo Hilo,Makamu Wa Rais Huyo
Alitoa Wito Kwa Wakenya Wote Kuunga Mkono Serikali Ya Kenya Kwanza.
Mheshimiwa Gachagua Ambaye
Amekuwa Akipiga Kambi Katika Kaunti Ya Uasin Gishu Kwa Siku Tatu Zilizopita
Alisema Amejitolea Kumuunga Mkono, Rais Dkt.Ruto Katika Azma Yake Ya
Kuwaunganisha Wakenya Wote.
“Nimekuwa Katika Kaunti
Hii Kwa Siku Tatu Zilizopita Kwa Sababu Ya Maendeleo Na Kuwashukuru Kwa Kuunga
Mkono Serikali Yetu.
"Jukumu Letu Kuu Ni
Kuwaunganisha Wakenya Wote Ili Kuchochea Maendeleo,” Alisema Makamu Wa Rais, Gachagua
Akihutubia Katika Soko La Burnt Forest Baada Ya Harambee. (NA)