JAMHURI Ya Kidemokrasia Ya
Kongo Imeiteuwa Serikali Mpya, Na Hivyo Kuhitimisha Mkwamo Ambao Umeikumba Nchi
Hiyo Katika Sintofahamu Ya Kisiasa Kwa Miezi Kadhaa.
Katika Tangazo
Lililotolewa Mapema Leo Na Msemaji Wa Serikali Tina Salama Na Kurushwa Na
Televisheni Ya Taifa RTNC, Baraza Hilo Jipya Lina Mawaziri 54 Ikilinganishwa Na
57 Katika Serikali Iliyopita. Mwanasheria Guy Kabombo Muadiamvita Ameteuliwa
Kuwa Waziri Wa Ulinzi - Wadhifa Muhimu Ikizingatiwa Mgogoro Mbaya Kabisa Wa
Miaka Miwili Kati Ya Kongo Na Waasi Wa M23 Mashariki Mwa Nchi Hiyo.
Doudou Fwamba Likunde Ameteuliwa
Waziri Wa Fedha Na Kizito Pakabomba Atasimamia Wizara Muhimu Ya Madini. Akirejelea
Kucheleweshwa Kuundwa Serikali, Mkurugenzi Wa Mawasiliano Wa Rais Erik Nyindu Alisema
Ilichukua Muda Kwa Pande Tofauti Katika Muungano Tawala Kufikia Maelewano.
Rais Felix Tshisekedi Alishinda
Muhula Wa Pili Baada Ya Uchaguzi Wa Mwishoni Mwa Mwaka Wa 2023 Ambao Uliupa
Muungano Wa Union Sacre Wingi Mkubwa Wa Viti Bungeni. Lakini Malumbano Ya Ndani
Ya Kugombania Nyadhifa Yakachelewesha Kuundwa Kwa Baraza Jipya La Mawaziri.
Rais Hatimaye Alimtangaza Judith Suminwa Kuwa Waziri Mkuu Wa Kwanza Mwanamke Nchini Kongo Na Aliyekuwa Mkuu Wake Wa Utumishi Vital Kamerhe Kuwa Spika Wa Bunge Na Hivyo Kusafisha Njia Ya Kuteuliwa Serikali.