MAKUMI Kwa Maelfu Ya
Waandamanaji Walikusanyika Jana Katikati Ya Mji Mkuu Wa Armenia, Yerevan,
Wakimtaka Waziri Mkuu Nikol Pashinyan Ajiuzulu.
Hii Ni Baada Ya Armenia Kukubali
Kuikabidhi Azerbaijanudhibiti Wa Vijiji Kadhaa Vya Mpakani. Maandamano Hayo
Yalikuwa Ya Karibuni Katika Wiki Ya Msururu Wa Mikusanyiko Iliyoongozwa Na
Mhubiri Mashuhuri Katika Kanisa La Mitume La Kiarmenia, Bagrat Galstanyan,
Askofu Mkuu Wa Jimbo La Tavush, Kaskazini Mashariki Mwa Armenia.
Aliongoza Kuundwa Kwa
Vuguvugu Linalojulikana Kama Tavush For The Homeland Vaada Ya Armenia Mnamo Aprili
Kukubali Kuwachia Udhibiti Wa Vijiji Vinne Katika Eneo La Azerbaijan. Ijapokuwa
Vijiji Hivyo Vilikuwa Suala Kuu La Kuundwa Vuguvugu Hilo, Limetanuka Na
Kuelezea Malalamiko Mengine Kuhusu Pashinyan Na Serikali Yake.
Viongozi Wa Vuguvugu Hilo
Wameuambia Mkutano Wa Jana Kuwa Wanaunga Mkono Galstanyan Kuwa Waziri Mkuu
Mpya. Uamuzi Wa Kuvikabidhi Vijiji Hivyo Vya Tavush Ulifuatia Operesheni Kali
Ya Kijeshi Septembamwaka Jana Ambapo Jeshi La Azerbaijan Liliwalazimu Maafisa
Wa Kiarmenia Wanaopigania Kujitenga Katika Mkoa Wa Karabakh Kusalimu Amri.