KUNA
Faida Za Kiafya Za Kunywa Chai Ambazo Labda Huzijui. Chai Ni Mojawapo Ya
Vinywaji Vinavyotumiwa Sana Duniani Na Imekuwa Ikitumiwa Kwa Karne Nyingi.
Kuna
Aina Tofauti Za Chai; Nyeusi, Kijani, Nyeupe Na Rangi Zingine. Kila Moja Ina
Ladha Yake Ya Kipekee Na Sifa Na Aina Ya Jani La Chai Na Usindikaji Wake.
Mei
21 Pia Huadhimishwa Kama Siku Ya Chai Duniani. Je, Chai Ina Faida Gani Kwa Afya
Ya Binaadamu?
Faida Nane Za Chai
Kunywa Chai Kunaweza
Kuboresha Jinsi Mishipa Yetu Ya Damu Inavyofanya Kazi Na Kupunguza Shinikizo La
Damu.
Huongeza Upatikanaji Wa
Kitu Kiitwacho Nitriki Oksidi, Ambayo Husaidia Kulegeza Misuli Katika Mishipa
Yetu Ya Damu Na Kuruhusu Damu Kutiririka Kwa Uhuru Katika Mwili Wote.
Kupunguza Hatari Ya
Mshtuko Wa Moyo
Ushahidi Unaonyesha
Unywaji Wa Chai Mara Kwa Mara Unaweza Kupunguza Hatari Ya Mshtuko Wa Moyo Na
Hii Ni Kutokana Na Kemikali Ya Polyphenol Katika Chai.
Chai Ya Kijani Inaonekana
Kuwa Yenye Ufanisi Zaidi Linapokuja Suala Hili.
Kupunguza Kisukari
Kulingana Na Utafiti,
Matumizi Ya Mara Kwa Mara Ya Polyphenols Katika Chai Ya Mitishamba Inaweza Kuwa
Na Ufanisi Kupunguza Hatari Ya Ugonjwa Wa Kisukari.
Lakini Utafiti Zaidi
Unahitajika Katika Eneo Hili.
Kuboresha Utendaji Wa
Tumbo
Aina Nyingi Za
Polyphenols Katika Chakula, Ikiwa Ni Pamoja Na Chai, Hutoa Chanzo Muhimu Cha
Bakteria Wa Tumbo Wenye Manufaa, Inawasaidia Kukua Na Kuboresha Utendaji Wa
Tumbo.
Kupunguza Saratani
Kemikali Za Polyphenols Zinazopatikana
Katika Chai Zinaweza Kufanya Kazi Ya Kupunguza Ukuaji Wa Aina Fulani Za
Saratani.
Ushahidi Uliopatikana Ni
Wa Saratani Ya Mdomo Na Aina Zingine Za Saratani Kama Vile Ini, Matiti Na
Koloni.
Kupunguza Wasiwasi Na
Uchovu
Tofauti Na Kahawa, Ambayo
Inachukuliwa Kuwa Kinywaji Kikali, Chai Kwa Ujumla Inachukuliwa Kuwa Kinywaji
Laini.
Ingawa Zote Zina Kafeini,
Chai Ina Vitu Ambavyo Ni Laini Kuliko Kahawa, Humtuliza Mtu Kutokana Na Uwezo
Wake Wa Kuongeza Mawimbi Ya Ubongo Ya Alpha.
Kuongeza Umakini
Vinywaji Vilivyo Na
Kafeini Na Kemikali Ya L-Theanine Vyote Vina Umuhimu Kwenye Kuongeza Umakini.
Kikombe Kimoja Cha Chai
Ya Kijani Hutoa Miligramu 25 Za L-Theanine Na Husaidia Kutunza Kumbukumbu. Inatusaidia
Kuwa Macho.
Sio Kwamba Chai Ya Kijani
Ina Faida Pekee, Tathmini Mpya Juu Ya Chai Nyeusi Inaeleza Kuboresha Kumbukumbu
Pia.
Kupunguza
Maumivu Ya Mifupa
Kuna Ushahidi Kunywa
Chai, Hasa Chai Ya Kijani, Inaweza Kusaidia Kuzuia Matatizo Ya Mifupa Na
Kupunguza Hatari Ya Kupasuka.
Kuna Tafiti Mbili Tofauti
Kuhusu Kuweka Maziwa Kwenye Chai Nyeusi. Baadhi Wanasema Inaweza Kuathiri Uwezo
Wa Polyphenols Na Kuathiri Faida Ya Kiafya Ya Chai.
Lakini Katika Tafiti
Zingine, Kuongeza Maziwa Kwenye Chai Hakuna Athari. Inaonekana Kuongeza Maziwa
Kidogo Na Sukari Kwenye Chai Hakuibadilishi Sana Faida Za Chai. Lakini Kuongeza
Kiasi Kikubwa Cha Maziwa Kunaweza Kuathiri Faida Ya Chai.
Sukari Inayoongezwa
Katika Vinywaji Vya Moto Kama Vile Chai Inachukuliwa Kuwa 'Sukari Isiyofaa',
Kwa Hivyo Madaktari Wanapendekeza Uepuke Kuweka Sukari Nyingi Kupita Kiasi.
Kwa Wastani, Kwa Mtu
Ambaye Hana Tatizo Na Kafeini, Vikombe Vitatu Hadi Vinne Vya Chai Nyeusi Kwa
Siku Vinaweza Kuwa Kiasi Kinachofaa, Lakini Mtu Anayependa Chai Ya Kijani
Anapaswa Kunywa Chini Ya Hapo.
Ikiwa Una Shida Na
Kafeni, Inashauriwa Kupunguza Kiasi Cha Vinywaji Vya Kafeini, Ikiwa Ni Pamoja
Na Chai.
Kunywa Chai Nyingi
Kunaweza Kuharibu Usingizi Wako Na Kusababisha Wasiwasi Kwa Baadhi Ya Watu.
Watu Wengine Ambao
Wanapaswa Kupunguza Utumiaji Wa Kafeni Ni Wanawake Wajawazito.