MAWAZIRI Wa Ulinzi Wa Umoja
Wa Ulaya Waliokutana Mjini Brussels Walishindwa Kufikia Makubaliano Kuhusu Kama
Ukraine Inapaswa Kuruhusiwa Kutumia Silaha Wanazoipa, Kuyapiga Maeneo Ndani Ya Urusi.
Nchi Za Umoja Wa Ulaya Zilikuwa
Tayari Zimekubali Kwa Pamoja Kutoa Msaada Wa Kijeshi Kwa Ukraine. Lakini Wakati
Baadhi Ya Wanachama Wanatoa Silaha Kwa Kyiv Zikiandamana Na Vikwazo Kidogo,
Wengine Wanafanya Hivyo Kwa Masharti Kuwa Zitatumika Ndani Ya Mipaka Ya Ukraine.
Lakini Serikali Ya Ukraine
Inasema Wanajeshi Wake Wanahitaji Kuyapiga Maeneo Ndani Ya Urusi, Kwa Sababu Urusi
Inaanzisha Mashambulizi Kutokea Nchini Mwake.
Mkuu Wa Sera Za Kigeni Wa
Umoja Wa Ulaya Josep Borrell Amesema Katika Kikao Cha Waandishi Wa Habari Baada
Ya Mkutano Huo Kuwa Matumizi Ya Mashambulizi Ya Kujilinda Dhidi Ya Maeneo Ya
Kijeshi Katika Ardhi Ya Urusi "Ni Kitendo Halali Chini Ya Sheria Za
Kimataifa Wakati Inapotumiwa Kwa Usawa."
Lakini Pia Ni Wazi Kuwa
Ni Uamuzi Wa Binafsi Wa Kila Mwanachama Wa Umoja Wa Ulaya. Borrell Amesema
Hakuna Anayeweza Kumzuia Nchi Mwanachama Kutoa Silaha Kwa Ukraine Na Kuwaruhusu
Waukraine Kuzitumia Silaha Hizo Kuyalenga Maeneo Ya Kijeshi Ndani Ya Urusi. Lakini
Pia Umoja Wa Ulaya Hauwezi Kuwalazimisha Kufanya Hivyo.
Kwingineko, Rais Wa Ufaransa
Emmanuel Macron Anaunga Mkono Ukraine Kuruhusiwa Kutumia Silaha Za Magharibi Kuyashambulia
Maeneo Ya Urusi Katika Ardhi Ya Urusi. Akizungumza Baada Ya Kukutana Na Kansela
Wa Ujerumani Olaf Scholz Karibu Na Mji Mkuu Berlin, Macron Amesema Ni Muhimu
Kuiruhusu Ukraine Kuviangamiza Vituo Vya Kijeshi Ambavyo Vinatumika Kufyatua
Makombora Yanayoelekezwa Ndani Ya Ukraine.
Wakati Huo Huo, Rais Wa Urusi
Vladmir Putin Amesema Kuwa Kutakuwa Na Kile Alichokiita "Madhara Makubwa”
Kama Nchi Za Magharibi Zitairuhusu Ukraine Kutumia Silaha Zao Kuyapiga Maeneo
Ndani Ya Urusi, Kama Inavyotaka Kyiv. Putin Amesema Barani Ulaya Na Hasa Nchi
Ndogo, Zinapaswa Kufahamu Zinachokichezea, Akibainisha Kuwa Nchi Nyingi Za Ulaya
Zina Maeneo Madogo Na Idadi Kubwa Ya Watu. Amesema Hata Kama Askari Wa Ukraine Watafanya
Mashambulizi Hayo, Wauzaji Wa Silaha Kutoka Nchi Za Magharibi Ndio
Watakaowajibishwa.
Nchi Za Umoja Wa Ulaya Zimegawanyika
Pia Kuhusu Kama Watoa Mafunzo Ya Kijeshi Kutoka Umoja Wa ULAYA Wanapaswa
Kuruhusiwa Kutoa Mafunzo Kwenye Ardhi Ya Ukraine, Au Kama Askari Wa Ukraine Wanapaswa
Kupelekwa Katika Umoja Wa Ulaya Kupewa Mafunzo.
Putin Pia Amesema Kuwa
Wakati Anaamini Watoa Mafunzo Ya Kijeshi Wa Magharibi Wako Tayari Ukraine Wakihudumu
Kisiri Kama Mamluki, Hatua Yoyote Ya Nchi Kuwatuma Rasmi Nchini Humo Itakuwa
Hatua Nyingine Ya Kuongeza Mvutano Na Hatua Nyingine Kuelekea Mgogoro Mkubwa
Barani Ulaya, Kuelekea Mgogoro Wa Kimataifa.
Baadhi Wanahofia Kuwa
Kuwapeleka Askari Nchini Ukraine Kunaweza Kuongeza Kushiriki Kwao Katika Vita
Na Kuongeza Hatari Ya Kuzuka Mgogoro Wa Moja Kwa Moja Kati Ya Urusi Na Nchi Za Magharibi.
Hata Hivyo, Mawaziri Hao
Wa Ulinzi Waliweza Kukubaliana Kuhusu Masuala Ya Kipaumbele Kwa Ulinzi Wa Ulaya
Katika Mkutano Huo. Walitangaza Uungaji Mkono Wa Umoja Wa Ulaya Usioyumba Kwa Ukraine
Ambapo Umoja Huo Utatumia Nyenzo Zote Ilizo Nazo. Miongoni Mwazo Ni Mfuko Wa
Nje Ya Bajeti Unaoitwa Hazina Ya Amani Barani Ulaya Ambapo Umoja Wa Ulaya Umeahidi
Dola Bilioni 5.4 Za Msaada Wa Kijeshi Kwa Ukraine. Serikali Ya Uholanzi Imesema
Itaongoza Mpango Wa Baadhi Ya Nchi Ta Ulaya Ili Kuipa Ukraine Mfumo Wa Ulinzi
Wa Angani Aina Ya Patriot.
Pia Kwenye Orodha Ya
Vipaumbele Vya Mawaziri Hao Wa Ulinzi Ni Kuimarisha Uwezo Wa Kiviwanda Wa Umoja
Wa Ulaya Kutengeneza Zana Za Kivita Na Teknolojia Ya Ulinzi.