TAJIRI zaidi duniani, Elon Musk, hajaalikwa
kwenye Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji wa serikali ya Uingereza ikiwa ni
hatua ya kujibu ujumbe wake kwenye mitandao ya kijamii wakati wa ghasia za
mwezi uliopita.
Ghasia zilienea kote Uingereza baada ya shambulio la kisu
huko Southport, ambapo watoto watatu waliokuwa wakihudhuria darasa la kucheza
densi waliuawa.
Mjasiriamali huyo wa teknolojia aliweka kwenye mtandao wa X,
ambao zamani ulijulikana kama Twitter, ujumbe akitabiri vita vya wenyewe kwa
wenyewe nchini Uingereza na kumshambulia mara kwa mara waziri mkuu.
Mkutano wa kilele mwezi Oktoba ni wakati muhimu ambapo Waziri
Mkuu Keir Starmer anatumai kuvutia makumi ya mabilioni ya fedha kwa ajili ya
biashara kutoka kwa wawekezaji wakubwa duniani.
Bw Musk alihudhuria hafla ya mwaka jana na kuchukua jukumu
muhimu katika mkutano wa akili mnemba - AI wa Novemba, ikiwa ni pamoja na
mazungumzo ya kusisimua ya pembeni na Waziri Mkuu wa wakati huo Rishi Sunak.
Serikali na Bw Musk wametafutwa ili kutoa maoni yao.
Wakati wa ghasia za Agosti, Bw Musk alishirikisha, na baadaye
kufuta maoni yake kuhusu fikra za njama ya Uingereza kujenga "kambi za
kizuizini" katika Visiwa vya Falkland kwa ajili ya waasi, kwenye mtandao
wa X - jukwaa analomiliki.
Wakati huo mawaziri walisema maoni yake "hayana msingi
wowote" na ni "ya kusikitisha sana."
Huenda hii ndiyo sababu hajaalikwa kuungana na mamia ya
wawekezaji wakubwa duniani katika hafla hiyo ya tarehe 14 Oktoba.
JISAJIRI
SASA NA PLAY MASTER BET - BETI KIRAHISI
BONYEZA
HAPA KUJISAJIRI