MAREKANI YASEMA IRAN ILITUMA TAARIFA ZA UDUKUZI KUMHUSU TRUMP KWA WASHIRIKA WA BIDEN


WADUKUZI wa Iran walisambaza taarifa za udukuzi kuhusu kampeni ya uchaguzi ya Donald Trump kwa watu wanaohusika na kampeni ya Biden, kulingana na FBI na mashirika ya kijasusi ya Marekani.

Maafisa wa Marekani sasa wanaamini kwamba taarifa zilizochukuliwa kutoka kwa kampeni ya Trump zilitumwa kwa barua pepe kwa watu wanaohusika na kampeni mwishoni mwa mwezi Juni na mapema mwezi Julai kabla Biden hajajiondoa kwenye kinyang'anyiro cha urais.

Kwa sasa hakuna ushahidi kwamba wavamizi hao walipokea jibu lolote kutoka kwa wapokeaji wowote wa taarifa hizo.

Mwezi Agosti, maafisa walitahadharisha kwamba Iran inatarajia "kuchochea mifarakano" na kudhoofisha imani kwa taasisi za Marekani kabla ya uchaguzi wa mwezi Novemba.

Maafisa wa Marekani walisema kuwa Iran imetumia "uhandisi wa kijamii na juhudi nyingine" kutafuta ufikiaji wa moja kwa moja kwa kampeni za Democrat na Republican, mbinu ambayo walisema imetumiwa na Iran na Urusi katika nchi nyingine ulimwenguni.

 

JISAJIRI SASA NA PLAY MASTER BET - BETI KIRAHISI

BONYEZA HAPA KUJISAJIRI



Previous Post Next Post

ADVERT

ADVERT