WAAFRIKA Kusini Wanapiga
Kura Kulichagua Bunge Jipya, Katika Uchaguzi Ambao Huenda Ukafungua Ukurasa
Mpya Nchini Humo. Chama Tawala ANC, Kipo Katika Hatari Ya Kupoteza Wingi Wake
Wa Viti Bungeni.
Uchaguzi Huo Unaonekana
Kama Ndio Muhimu Zaidi Tangu Mpigania Uhuru Na Kisha Baadae Rais Nelson Mandela
Alipoiongoza Nchi Hiyo Kupata Demokrasia Mwaka Wa 1994.
Chama Cha African
National Congress - ANC, Ambacho Kimetawala Afrika Kusini Mfululizo Tangu
Kumalizika Kwa Enzi Ya Ubaguzi Wa Rangi, Kipo Katika Hatari Ya Kupoteza Wingi
Wake Wa Viti Bungeni Kwa Mara Ya Kwanza Tangu Wakati Huo. Kwa Mujibu Wa
Uchunguzi Wa Maoni, ANC Inatarajiwa Kupata Chini Ya Asilimia 50 Ya Kura Na
Itahitajika Kuunda Serikali Ya Muungano.
Afrika Kusini Inakabiliwa
Na Uchumi Unaodhoofika, Ukosefu Mkubwa Wa Ajira Na Umaskini, Kukatika Kwa Umeme
Mara Kwa Mara, Na Huduma Mbovu Za Usambazaji Maji, Mfumo Unaoporomoka Wa Huduma
Za Afya Pamoja Na Viwango Vya Juu Vya Uhalifu Na Mfumo Wa Haki Ya Jinai
Usiofanya Kazi. Wanachama Wa Vyama 52 Wanashindania Viti 400 Katika Bunge La
Kitaifa.
Serikali Mpya Za Mikoa
Pia Zitachaguliwa. Kati Ya Watu Milioni 40.1 Wenye Uwezo Wa Kupiga Kura, Ni
Milioni 27.4 Ambao Wamesajiliwa Kupiga Kura. Bunge Jipya Litakalochaguliwa
Lazima Kisha Liunde Serikali Na Kumchagua Rais Katika Kipindi Cha Siku 14.