VIFARU Vya Israel Vimeendelea
Kushambulia Katika Mji Wa Rafah Kwa Siku Ya Pili Leo Na Kukaidi Uamuzi
Uliotolewa Na Mahakama Ya Kimataifa Ulioitaka Nchi Hiyo Isitishe Hatua Ya
Kuushambulia Mji Huo Wa Kusini Mwa Gaza.
Israel Imeendeleza
Mashambulizi Hayo Leo Baada Ya Marekani Kusema Hatua Zinazochukuliwa Na Israel Hazijafikia
Operesheni Kubwa Za Kijeshi Katika Mji Huo.Marekani Iliitahadharisha Israel Kuepuka
Kufanya Mashambulizi Makubwa.
Jana Ni Mara Ya Kwanza Israel
Kupeleka Vifaru Katikati Ya Mji Wa Rafah Licha Ya Mahakama Ya Kimataifa Inayosimamia
Haki,Iliyoko Nchini Uholanzi Kuitaka Isitishe Mashambulizi Kwenye Mji Huo.
Israel Kuendeleza Vita Gaza
Hadi Mwishoni Mwa Mwaka 2024
Wakaazi Wa Rafah Wamesema
Vifaru Hivyo Vya Kijeshi Vya Israel Viliingia Hadi Magharibi Mwa Mji Huo Kabla
Ya Kuelekea Kwenye Eneo La Usalama Lililowekwa
Lililoko Katika Mpaka Na Misri.