RAIS Wa Marekani Joe
Biden Amesema Ilikuwa "Uzembe" Kwa Mtangulizi Wake, Donald Trump,
Kuitaja Kesi Yake Kuwa Na Udanganyifu, Siku Moja Baada Ya Kupatikana Na Hatia
Na Kuweka Kihistoria Nchini Humo.
Akizungumzia Maoni Ya
Kwanza Kwa Umma Ya Trump Kuhusu Kupatikana Na Hatia Kwa Makosa 34 Ya Kughushi
Rekodi Za Biashara, Bw. Biden Alitetea Mfumo Wa Sheria Wa Marekani.
"Kanuni Ya Marekani Kwamba
Hakuna Mtu Aliye Juu Ya Sheria Ilithibitishwa Tena," Bw Biden Alisema
Kuhusu Kilichotokea.
Mapema Siku Ya Ijumaa, Trump
Alitoa Maneno Makali Kwenye Mkutano Na Wanahabari Katika Jengo La Trump Tower Huko
Manhattan, Akimtaja Jaji Kuwa "Mpotovu", Kesi Hiyo Ni
"Uzushi" Na "Majambazi" Wa Democrats.
Maoni Ya Bw Biden Siku Ya
Ijumaa Alasiri Yanawadia Mwanzoni Mwa Mkutano Wa Waandishi Wa Habari Wa White
House Ambapo Alijadili Mashariki Ya Kati Na Pendekezo Jipya La Israel Kwa Gaza.
Bw Biden Alisema Mpinzani
Wake Wa Chama Cha Republican Katika Uchaguzi Wa Rais Wa Mwezi Novemba Alikuwa
Amepewa "Kila Fursa" Ya Kujitetea, Na Haikuwa Sawa Kulalamika Kwamba
Mchakato Huo Haukuwa Wa Haki.
"Ni Uzembe. Ni Hatari.
Ni Kutowajibika Kwa Mtu Yeyote Kusema Kuwa Hii Ilipangwa Kwa Sababu Tu
Hawapendi Uamuzi Huo," Alisema Na Kuongeza Kuwa Trump Anakaribishwa
Kuwasilisha Rufaa.
Bw Biden, Ambaye
Amezungumza Mara Chache Sana Hadharani Kuhusu Matatizo Ya Kisheria Ya Trump,
Alisema Mfumo Wa Sheria Ndio "Msingi Wa Marekani".
"Mfumo Wa Sheria
Unapaswa Kuheshimiwa Na Kamwe Tusiruhusu Mtu Yeyote Kuubomoa. Ni Rahisi Tu
Namna Hiyo. Hiyo Ndio Marekani. Ndivyo Tulivyo," Alisema.