JESHI La Polisi Mkoani Songwe
Linamshikilia Mwanamke Mmoja Na Mtu Mwingine Anayedaiwa Ni Hawara Yake Kwa
Tuhuma Za Mauaji Ya Mme Wa Mwanamke Huyo Kwa Kile Kinachodaiwa Ni Wivu Wa
Mapenzi.
Watuhumiwa Hao Ambao
Majina Yao Hayajatajwa Wanadaiwa Kumuua Victor Mwakapenda (41), Mkazi Wa Mtaa
Wa Ilembo, Mbozi Mkoani Humo.
Kamanda Wa Polisi Mkoani
Humo, Augustino Senga Amethibitisha Kutokea Kwa Tukio Hilo Na Kuwa Uchunguzi Wa
Awali Umebaini Kuwa Chanzo Cha Mauaji Hayo Ni Wivu Wa Mapenzi.
Kamanda Senga Amesema
Marehemu Alitoweka Nyumbani Tangu Aprili 30 Mwaka Huu Akiwa Na Mke Wake Na
Mwili Wake Kuokotwa Mei 9, Mwaka Huu Katika Msitu Wa Mpoloto Uliopo Kijiji Cha Igale
Mbeya Vijijini.
Amesema Baada Ya Kuukuta,
Mwili Huo Ulipelekwa Kwenye Hospitali Ya Ifisi Jijini Mbeya Na Kuhifadhiwa
Mpaka Ndugu Zake Walipoutambua Na Kukabidhiwa Mei 29 Mwaka Huu.
Kamanda Senga Amesema
Mpaka Sasa Wanawashikilia Watu Wawili Wanaosadikiwa Kuhusika Na Tukio Hilo,
Akiwepo Mke Wa Marehemu Na Dereva Mmoja Wa Pikipiki, Lakini Hakuwataja Akisema
Bado Wapo Kwenye Uchunguzi.
"Ni Kweli
Tunawashikilia Watu Wawili Ambao Inadaiwa Walikuwa Na Uhusiano Na Siku Ambayo
Marehemu Alitoweka Nyumbani, Dereva Huyo Bodaboda Ndiye Aliyembeba Na Mke Wake
Akiwepo, Hivyo Uchunguzi Unaendelea," Amesema Kamanda Senga.
Akizungumza Na Mwananchi,
Mjumbe Wa Shina Namba Moja Mtaani Hapo, Aliki Songa Amesema “Sisi Tunasikitika
Kwa Mauaji Ya Mwenzetu Na Kifo Chake Kinahusishwa Na Wivu Wa Mapenzi Kati Ya
Marehemu Na Mke Wake”.
"Tunashukuru Jeshi La
Polisi Kuwashikilia Watu Hawa, Kwani Sisi Kama Wananchi Hatujawahi Kushuhudia
Tukio La Namna Kama Hili, Hivyo Kama Unaona Umechoka Kukaa Na Mwenzako Bora
Uachane Naye Kuliko Kusababisha Kifo, Ni Mbaya Sana," Amesema Songa.
Akizungumza Msibani Hapo,
Kaka Wa Marehemu Aliyejitambulisha Kama Mwakapenda Amesema Kifo Cha Mdogo Wake
Hakivumiliki Na Kama Walikuwa Na Ugomvi Wangemfikisha Kwenye Vyombo Vya Sheria
Kuliko Kumuua Kinyama.