VIONGOZI
Wa Kundi La Nchi Saba Zilizostawi Kiviwanda Duniani, G7 Wanafanya Mkutano Wao
Wa Kilele Nchini Italia, Na Wamefikia Makubaliano Ya Kuipa Ukraine Msaada
Zaidi.
Kwa
Mwaka Wa Pili Mfulilizo, Rais Wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy Atahudhuria
Mkutano Huo, Akishiriki Katika Mazungumzo Hayo Leo Alhamisi.
Rais
Zelensky Amesema Anatarajia "Maamuzi Muhimu" Katika Mkutano Huo
Ambapo Pia Atatia Saini Makubaliano Ya Usalama Na Japan Na Marekani.
Viongozi
Wa G7 Wanatarajia Kutangaza Angalau Kimsingi Mpango Wa Kuipa Ukraine Mkopo
Wa Dola Bilioni 50 Kwa Kutumia Riba Inayotokana Na Mali Za Urusi Zilizozuwiwa
Baada Ya Uvamizi Wake Nchini Ukraine.
Tatizo
La Kisheria
Hata
Hivyo Viongozi Hao Wanakiri Kwamba Mpango Huo Ni Mgumu, Huku Wataalamu Wa
Sheria Wakitakiwa Kushughulikia Maelezo Ambayo Watahitaji Ili Kuungwa Mkono Na
Mataifa Ya Ulaya, Hasa Ubelgiji, Ambayo Siyo Mwanachama Wa Kundi La G7.
Miongoni
Mwa Agenda Kuu Za Mkutano Ni Pamoja Mzozo Wa Mashariki Ya Kati, Uhamiaji Na
Teknolojia Za Akili Ya Kubuni Katika Wakati Ambapo Wengi Wao Pia Wanakabiliwa
Na Changamoto Mbalimbali Katika Mataifa Yao.
Mwenyeji
Wa Mkutano Huu Waziri Mkuu Wa Italia Giorgia Meloni Pekee Anaweza Kushusha
Pumzi Baada Ya Kushinda Katika Uchaguzi Wa Ulaya Italia Mwishoni Mwa Wiki.
Katika
Kutilia Mkazo Azma Ya Marekani Kuiadhibu Moscow Kwa Sababu Ya Uvamizi Kamili
Dhidi Za Ukraine, Washington Siku Ya Jumatano Ilipanua Vikwazo Kwa Moscow, Ikiwa
Ni Pamoja Na Kulenga Makampuni Ya Vifaa Vya Teknolojia Ya China Kuuza Bidhaa
Zake Kwa Moscow.
Kwa
Kutangaza Vikwazo Vipya Kwa Makampuni Za China Siku Mmoja Kabla Za Kuanza Rasmi
Kwa Mkutano Wa G7, Biden Bila Shaka Ana Matumaini Ya Kuwashawishi Washirika Wa Magharibi
Kuonyesha Dhamira Kubwa Katika Kukabiliana Na Beijing Kuiunga Mkono Urusi Na
Hatua Yake Za Kuzalisha Bidhaa Kwa Wingi Viwandani.
Huku
Haya Zakijiri Italia Inajaribu Kupuuza Tamko La G7 Kuhusu Uavyaji Mimba Kwa
Kuondoa Marejeleo Ya Usitishaji "Salama Na Wa Kisheria." Inaarifiwa Kuwa
Ya Pingamizi Kutoka Kwa Waziri Mkuu Wa Mrengo Wa Kulia Giorgia Meloni Kuhusu
Kulinda Haki Za Ngono Zimewakasirisha Wanachama Wa Kundi Hilo Uingereza, Canada,
Ufaransa,Ujerumani, Japan Na Marekani.
Ofisi
Ya Meloni Jana Jumatano Ilipinga Haki Ya Utoaji Mimba Kupunguzwa Kutoka Kwa
Rasimu Ya Taarifa Ya Mwisho Ya Mkutano Huo, Ikisema Mazungumzo Yanaendelea.
JISAJIRI
SASA NA PLAY MASTER BET - BETI KIRAHISI
BONYEZA
HAPA KUJISAJIRI