WATU Saba Wamefariki Dunia Baada Ya Mtumbwi Waliokuwa Wakisafiria Kupasuka Kisha Kupinduka Halmashauri Ya Mlele, Kitongoji Cha Lungunya Mkoani Katavi.
Jeshi La Zimamoto Na Uokoaji
Mkoani Katavi Linaendelea Kuitafuta Miili Ya Watu Sita Kati Ya Saba Waliofariki
Dunia Katika Mto Ulipo Kitongoji Cha Lungunya, Halmashauri Ya Mlele, Mkoa Wa Katavi,
Walipokuwa Wakisafiri Kwa Kutumia Mtumbwi Uliopasuka Kisha Kupindua Ukiwa
Umebeba Watu 14 Na Magunia 10 Ya Mpunga.
Vifo Hivyo Vimetokea Hii
Jana Jumapili, Mei 26, 2024 Ambapo Inaelezwa Mtumbwi Ulikuwa Umebeba Watu 14 Na
Magunia 10 Ya Mpunga Hivyo Ukashindwa Kuhimili Uzito Huo.
Hadi Usiku Wa Jana Ni
Mwili Mmoja Umepatikana Huku Juhudi Zaidi Zikiendelea Kuipata Mingine Sita.
Kitongoji Cha Lungunya Wanatumia
Mitumbwi Kusafiri Kutokana Na Mvua Kubwa Zilizonyesha Na Kuharibu Miundombinu
Ya Barabara.
Mkazi Wa Eneo Hilo, Shija
Mwakahema Ameiomba Serikali Kukaa Chini Na Kuangalia Suala Hilo Kwani Mafuriko
Yanaendelea Na Yataendelea Na Kuiomba Serikakali Kukaa Chini Na Kuliangalia
Suala Hilo.
Kaimu Kamanda Wa Jeshi La
Zimamoto Na Uokoaji Mkoani Katavi, Lilian Wanna Alisema Katika Tukio Hilo
Wamefanikiwa Kutoka Watu Saba Kati Ya 14 Waliokuwa Wakisafiri.
“Asubuhi Tumefanikiwa
Kupata Mwili Mmoja Huku Miili Mingine Sita Bado Haijapatikana,” Alisema Kamanda
Lilian.
Alisema Wanaendelea
Kuwatafuta Huku Changamoto Ikiwa Eneo Hilo La Bonde Kuwa Na Mamba Pamoja Na
Viboko.
Kwa Upande Wake, Mkuu Wa Mkoa
Wa Katavi, Mwanamvua Mrindoko Amemwagiza Mkurugenzi Wa Halmashauri Ya Mlele Kufanywa
Tathmini Ya Eneo Hilo Kama Bado Ni Salama Kuishi Ili Kufahamu Maji Yaliyopo
Hapo Yanatoka Wapi.
“Tukisema Hapa Hapafai
Kwa Maisha Ya Mwanadamu Basi Mtuelewe, Pia Mchukue Tahadhari Kwa Ajili Ya
Kuepukana Na Vifo,” Alisema.