DR. SAULOS CHILIMA, Ni
Miongoni Mwa Watu 10 Waliokufa Katika Ajali Ya Ndege Ndogo Ya Kijeshi Iyoanguka
Katika Eneo La Milima Kaskazini Mwa Nchi Hiyo.
Rais Lazaro Chakwera Alitangaza
Katika Hotuba Ya Moja Kwa Moja Kwenye Televisheni Ya Taifa Kwamba Mabaki Ya
Ndege Hiyo Yalipatikana Baada Ya Kuitafuta Kwa Zaidi Ya Siku Moja Katika Msitu
Mnene Ulioko Eneo Milima Karibu Na Mji Wa Kaskazini Wa Mzuzu.Chakwera Alisema
Hakuna Mtu Aliyenusurika Ajali Hiyo.
"Maneno Hayawezi
Kueleza Jinsi Tukio Hili Linavyotuhuzunisha Nafikiria Juu Ya Uchungu Tulionao
Na Tukaokuwanao Sote Katika Siku Na Wiki Zijazo Tunapoomboleza Msiba Huu Mbaya.
Ni Muhimu Tuendelee Kufarijiana Wakati Tunapoomboleza Kwa Pamoja. Dr Saulos
Chilima Alikuwa Mtu Mwema, Baba Mzuri Na Mume Aliyejitolea, Raia Mzalendo
Aliyeitumikia Nchi Yake Kwa Upendo, Na Makamu Wa Rais Asiye Na Mfano. Ni Heshima
Kubwa Maishani Mwangu Kufanyakazi Na Yeye Kama Naibu Wangu Na Mshauri Wangu Pia
Kwa Miaka Minne Iliyopita.” Alisema Chikwera.
Bibi Shanil Dzimbiri, Mke
Wa Rais Wa Zamaniwa Malawi Bakili Muluzi, Pia Alikuwa Ndani Ya Ndege Hiyo. Chakwera
Amesema Kulikuwa Na Abiria Saba Na Wafanyakazi Watatu Wanajeshi Kwenye Ndege
Hiyo.
Kundi Hilo Lilikuwa
Likisafiri Kuelekea Mzuzu Kuhudhuria Mazishi Ya Waziri Wa Zamani. Dr. Chilima Amefariki
Akiwa Na Umri Wa Miaka 51 Alikuwa Amerejea Kutoka Katika Kwenye Ziara Rasmi
Nchini Korea Kusini Siku Ya Jumapili.