IDARA Ya Hali Ya Hewa
Nchini India Imeonya Kuwa Nchi Hiyo Inakabiliwa Na Wimbi La Pili La Joto Kalikatika Muda Wa Wiki Tatu,
Ikiwa Ni Pamoja Na Maeneo Ambayo Mamilioni Ya Watu Wanatazamiwa Kupiga Kura
Katika Uchaguzi Wa Wiki Sita.
Idara Ya Hali Ya Hewa Ya India
Imeelezea "Wasiwasi Wa Kiafya Wa Wastani" Kwa Watoto Wachanga, Wazee
Na Wale Walio Na Magonjwa Sugu, Na Kuwashauri Wakaazi Wa Majimbo Hayo Kuepuka
Kukaa Kwenye Maeneo Ya Joto. Mji Mkuu Wanew
Delhi Unatarajiwa Kuwa Na Viwango Vya Juu Vya Joto Vya 45C Mwishoni
Mwa Juma, Kulingana Na Utabiri.
Majimbo Ya Uttar Pradesh,
Bengal Magharibi, Maharashtra Na Jharkhand, Ambayo Yote Yatapiga Kura Siku Ya Jumatatu,
Yanatarajia Hali Ya "Wastani" Ya Joto Ikiwa Ni Pamoja Na Nyuzi Joto
40 C.
Katika Mji Wa Mathura,
Ulio Karibu Na New Delhi, Kiwango Cha Nyuzi Joto Kilivuka 41C Siku Ya Upigaji Kuramwishoni Mwa Mwezi Aprili,
Huku Takwimu Za Tume Ya Uchaguzi Zikionyesha Kupungua Kwa Wapiga Kura
Waliojitokeza Kwa Karibu Pointi Tisa Ukilinganisha Na Miaka Mitano Iliyopita.
Tume Ya Uchaguzi Ya India
Ilisema Mwezi Uliopita Ilikuwa Imeunda Jopokazi La Kukagua Athari Za Joto Kabla
Ya Kila Duru Ya Upigaji Kura.
Waziri Mkuu Wa India Narendra
Modi Aliwataka Wapiga Kura Mwezi Huu Kunywa "Maji Mengi Iwezekanavyo"
Siku Ya Kupiga Kura Katika Jimbo Lake La Nyumbani La Gujarat.
India Imekuwa Ikikabiliwa
Na Viwango Vya Joto Kali Wakati Wa Kiangazi Lakini Utafiti Wa Kisayansi
Umegundua Kwamba Mabadiliko Ya Tabianchi Yamesababisha Msimu Wa Joto Kuwa
Marefu, Wa Mara Kwa Mara Na Mkali Zaidi Katika Bara La Asia Na Duniani Kote.Indian Yarejea Kwenye Uchaguzi Katikati Ya
Kitisho Cha Joto
Mamilioni Ya Watu Katika
Maeneo Ya Kusini-Mashariki Mwa Asia Wamekabiliwa Na Wimbi La Joto La Muda Mrefu
Mwezi Uliopita Ambalo Lilisababisha Kufungwa Kwa Shule Nchini Ufilipino Na Bangladesh.
Dhoruba Kali Pia
Zimeshuhudiwa Katika Nchi Kadhaa Ikiwa Ni Pamoja Na Katika Mji Mkuu Wa Kifedha
Wa Mumbai, Ambapo Upepo Mkali Uliangusha Bango Kubwa Ambalo Liliua Watu 16 Na
Kuwaacha Makumi Ya Wengine Wamenaswa Chini Ya Mabaki.
Takriban Watu 11 Waliuawa
Katika Milipuko Ya Radi Wakati Wa Mvua Huko West Bengal Wiki Hii.